Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi ya timu ya baseball ya Chicago Cubs toka kwa mmiliki wa timu hiyo na Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea akipokea moja ya Tabuleti 61 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakipokea moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakiangalaia matumizi ya ya Tabuleti 61 katika darasa la kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.PICHA NA IKULU.
---
THE UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Serikali inakusudia kutoa maelfu kwa maelfu ya tabuleti za kufundishia masomo
mbali mbali kwa wanafunzi na walimu wa shule za sekondari nchini kama
njia ya ubunifu zaidi, ya kisayansi na ya uhakika ya kukabiliana na
changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kwa kutumia Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (ICT).
Ili kufanikisha mpango huo, Serikali inakusudia kuingia
ushirikiano (partnership) na taasisi
isiyokuwa ya kiserikali ya Opportunity Education Trust ya Marekani ambayo
leo, Jumatatu, Januari 27, 2014, inazindua mpango wa majaribio wa utoaji
wa tabuleti hizo kwa wanafunzi na walimu wao wa shule za sekondari nchini.
Mpango wa Serikali wa kusambaza tabuleti kwa wanafunzi
na walimu wa shule za sekondari ulitangazwa usiku wa jana, Jumapili,
Januari 26, 2013 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na kuzungumza na Bwana Joe
Ricketts, mwenye taasisi ya Opportunity Education Trust na mmoja wa
matajiri wa Marekani.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es
Salaam, Rais Kikwete amemweleza kwa undani Bwana Ricketts hatua ambazo
zimechukuliwa na Serikali yake kupania na kuboresha elimu tokea mwaka
2006, hatua ambazo zimechangia kupanua kwa kasi na kwa kiwango kikubwa
wigo wa utoaji elimu nchini na changamoto ambazo zimezuka kutokana na
upanuzi huo mkubwa.
Rais Kikwete amesema baadhi ya changamoto hizi ni
ukosefu wa walimu, na hasa walimu wa masomo ya sayansi, na ukosefu wa
vitabu vya kufundishia changamoto mbili kubwa ambazo zinatatuliwa na
matumizi ya tabuleti.
“Mbali na
upanuzi mkubwa wa nafasi za wanafunzi kupata elimu ya ngazi mbali mbali,
pia tumepanua sana ufundishaji wa walimu. Mwaka 2005, vyuo vyetu vyote
vilikuwa vinatoa walimu 500 sasa tunatoa walimu 12,000 kwa mwaka. Hivyo,
tunaamini kuwa katika mwaka mmoja ama miwili ijayo, tutakuwa tumemaliza
tatizo la walimu wa masomo ya sanaa,” Rais Kikwete alimwambia Ricketts na kuongeza:
“Lakini
bado tunakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi, kama zilivyo
nchi nyingine. Tuna upungufu wa walimu 26,000 na kwa mwaka vyuo vyetu
vyote vinahitimisha walimu 2,100 tu. Hii ina maana kuwa itabidi kusubiri
miaka 13 kuweza kumaliza tatizo hili kwa mahitaji ya sasa. Hili haliwezekani
na hii ndiyo maana halisi ya kutumia sayansi na teknolojia ya namna
hii kufundishia wanafunzi wetu.”
Rais Kikwete alisema kuwa matumizi ya teknolojia
kufundishia nchini ni jambo linalowezekana kwa urahisi kwa sababu mtandao
wa mawasiliano wa National Fibre Network
ambao karibu umefikia kila wilaya sasa.
Rais Kikwete alimshukuru Bwana Ricketts na
taasisi yake kwa kukubali kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchini
kwa kusambaza teknolojia ya kisasa kama moja ya njia za ubunifu zaidi
za kufundishia hasa masomo ya sayansi.
Chini ya mpango huo wa majaribio wa kusambaza teknolojia
hiyo ya kisasa, taasisi ya Opportunity Education Trust
inatoa tabuleti 1100 kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa sekondari katika
shule 33.
Bwana Ricketts ambaye ni mwenyeji wa Omaha, Nebraska
alimwambia Rais Kikwete: “Hapa tunafanya
majaribio na Tanzania ni nchi ya kwanza duniani miongoni mwa nchi ambazo
tunaunga mkono mipango ya maendeleo kunufaika na mpango huo wa majaribio.
Ni azma yetu kuwa baada ya kuwa tumefanya tathmini ya mafanikio na changamoto
za hatua hii ya majaribio, tutaupanua mpango huu kushirikisha shule
nyingi zaidi kwa kushirikiana na Serikali kwenye mpango wake mkubwa
wa kusambaza teknolojia hii katika shule zote za sekondari hapa Tanzania.”
Bwana Ricketts na wataalam wake pamoja na maofisa
wa Serikali wameanza kutekeleza mpango huo leo, Jumatatu, Januari 27,
2014, kwa kutoa tabuleti kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wama
Nakayama iliyoko Mkoa wa Pwani.
Baada ya leo, shughuli hiyo itahamia Zanzibar na
Pemba, kabla ya Bwana Ricketts na wataalam wake kutoa tabuleti kwa shule
zilizoko mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Kagera na Morogoro.
Shule zinazonufaika katika mpango huo ni za Serikali
na binafsi na kwa kuanzia masomo ambayo yanapatikana katika tabuleti
hizo ni hesabu, jiografia, historia na kiingereza.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
27 January, 2014
0 comments:
Post a Comment