SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, January 7, 2014

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal Waongoza Mamia Ya Waombolezaji Kuaga Mwili Wa Aliyekua Waziri wa Fedha na Uchumi Marehemu Dkt William Mgimwa Leo(Sunday 05,, January 2014) Jijini Dar es Salaam

 Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri Wakiwa Wanuingiza Mwili wa wa marehemu Dkt. William Mgimwa 

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014
  Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu na familia yake wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dkt William Mgimwa viwanja vya Karimjee hall jijini Dar es salaam leo january 5, 2014
 Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilala, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
  Mama Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho.
  Spika wa Bunge Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana heshima za mwisho
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, heshima za mwisho.
 Baadhi ya Mawaziri wakiwa katika foleni kuelekea kutoa heshima zao za mwisho.
Mawaziri wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. William Mgimwa wakati likipakiwa kwenye gari tayari kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa ndege kuelekea mkoani Iringa kwa maziko.
  Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika shughuli hiyo.
  Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria shughuli hiyo

0 comments:

Post a Comment