SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, January 3, 2014

Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto Kabwe na wakili wake, Albert Msando Watinga Mahakama Kuu Kupinga Kamati Kuu ya Chadema Kumjadili Zitto Kabwe hadi ombi lake la rufaa litakaposikilizwa,Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu nae atinga Mahakama Kuu

Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto (kulia) aktinga rasmi ofisi za  Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
 Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto(Kushoto)akiteta jambo  na wakili wake, Albert Msando wakitoka Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
 Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu (kushoto) na Wakili wa chama hicho, Peter Kibatala (katikati) wakitoka katika chumba cha Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto(Kulia)akifurahia jambo na wakili wake, Albert Msando wakitoka Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto(Kushoto) na wakili wake, Albert Msando wakitoka Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe akiwa na Mwanasheria wake,Albert Msando(katikati)na Mwanasheria wa Chadema,Peter Kibatara(kushoto) wakiwa nje chumba cha Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam jana wakisubiri maamuzi ya Jaji kuhusu madai ya Zitto ya Kupinga Kamati Kuu ya Chama hicho kumjadili
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana alitinga  mahakama kuu  kupinga kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya Chadema,Kikao ambacho kilikuwa kikutane leo.
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu(Kushoto)akiteta jambo na Mbunge wa Arusha Mjini -Godbless Lema.Picha na Fidelis Felix 
 ----- 
Mahakama Kuu Tanzania, imeizuia kwa muda Kamati Kuu ya Chadema kujadili ajenda zozote zinazomhusu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe hadi ombi lake la rufaa litakaposikilizwa.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji John Utamwa baada ya kupokea maombi ya Zitto kupitia kwa Wakili wake, Albert Msando kutaka rufaa yake aliyoiwasilisha Baraza Kuu kusikilizwa kwanza kabla ya kufanyika uamuzi mwingine.

Kamati Kuu ya chama hicho, ilipanga kukutana leo ikiwa na ajenda kuu tatu; kupanga mpangokazi wa chama kwa mwaka 2014, kupokea utetezi wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao na kupokea taarifa kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

Zuio la Mahakama

Zuio hilo lilikuja pia baada ya kutupiliwa mbali maombi ya pingamizi la Chadema lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Katiba na Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Peter Kibatala.

Akizungumza jana baada ya uamuzi huo wa Mahakama, Mwanasheria Mkuu Chadema, Tundu Lissu alisema hakuna jinsi zaidi ya kukubaliana na uamuzi huo... “Tumekubali kutokumjadili Zitto lakini tuliomba Mahakama iruhusu kuhojiwa kwa Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.

Zitto alifungua kesi Mahakama Kuu akiiomba iizuie Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Katibu Mkuu pamoja na Kamati Kuu ya Chadema kumjadili, kumchukulia hatua yoyote kuhusu uanachama wake hadi hapo rufaa yake aliyoikata Baraza Kuu la Chadema itakaposikilizwa.

Pia katika maombi yake, Zitto alitaka Mahakama kuzuia kwa njia yoyote, Kamati Kuu kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake ya Ubunge wa Kigoma Kaskazini.

Mbali na ombi hilo, pia aliiomba Mahakama kumwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie nakala ya mashtaka na maelezo ya uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu Novemba 22, 2013 wa kumwondolea nyadhifa zake ili aweze kuwasilisha rufaa yake Baraza Kuu la Chadema kupinga uamuzi huo.

Zitto kupitia wakili wake, Msando alifungua kesi hiyo ya madai namba moja ya mwaka 2014 akipinga uamuzi huo wa Novemba 22, 2013 pamoja na hatua zaidi zilizoagizwa kuchukuliwa dhidi yake kuhusiana na uanachama katika chama chake. Walalamikiwa ni Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chadema.

Walalamikiwa hao, kupitia kwa Lissu na Kibatala waliwasilisha pingamizi wakiiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo kwa madai kuwa vifungu vilivyotumiwa katika kuwasilisha maombi hayo havikuwa sahihi.

Pia waliomba Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo kwa madai kuwa hati ya kiapo iliyotumiwa kuwasilisha maombi hayo ina upungufu wa kisheria na kwamba Mahakama hiyo haina uwezo wa kuyasikiliza.
CHANZO HIKI HAPA BOFYA

0 comments:

Post a Comment