Mshindi
wa zawadi ya promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Juma Musa Ramadhani
akiwa ndani ya gari lake jipya aina ya Mitsubishi Double Cabin mara
baada kukabidhiwa rasmi katika hafla Maalum ya makabidhiano iliyofanyika
Mlimani City, Dar es salaam.
Msafara
wa kumsindikiza mshindi wa gari katika promosheni ya Pambika na Samsung
ukipita katika barabara ya Sam Nujoma kutokea eneo la Kibiashara la
Mlimani City kuelekea Tabata Segerea kwa Bw. Juma Musa Ramadhani
aliyeibuka mshindi katika droo ya mwisho ya promosheni ya Pambika na
Samsung.
Msafara
wa timu nzima ya Pambika na Samsung ukiwa katika mataa ya Tabata
kuelekea kwa mshindi wa gari huko Tabata Segerea. Mshindi alitangazwa
rasmi Jumatatu katika droo ya mwisho na Bw Juma Musa Ramadhani ambae ni
mfanyabiasahara akaibuka kidedea kwa kunyakua gari jipya la Mitsubishi
Double Cabin.
Hapa
ni mara baada ya kuwasili katika duka Bw. Juma Musa Ramadhani lililopo
maeneo ya Tabata Segerea. Kushoto ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa
Samsung Tanzania Bw. Sylvester Manyara akiwa na Mshindi wa Pambika na
Samsung katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Samsung
Tanzania.
Mshindi
wa droo kubwa ya promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Juma Musa
Ramadhan (46) amekabidhiwa rasmi zawadi yake ya gari aina ya Mitsubishi
Double Cabin toka kwa Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania
wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya gari hilo yaliyofanyika jijini
Dar es salaam.
Hatua
hiyo imekuja mara baada ya droo kubwa ya Pambika na Samsung
iliyochezeshwa siku ya Jumatatu ya wiki hii na kumtangaza Bw. Juma Musa
Ramadhani amabe ni mfanyabiashara kuwa mshindi wa Jumla wa promosheni
hiyo iliyodumu kwa muda wa wiki sita toka Novemba 7, 2013 mpaka Desemba
23, 2013.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa gari hilo rasmi, Bw Juma alisema kwamba gari
hilo limekuja wakati muwafaka ambapo atalitumia katika shughuli zake za
biashara ambazo zinaanza rasmi mwakani. “Nipo katika michakato ya mwisho
ya kufungua duka langu kubwa maeneo ya Tabata Segerea ambako ndiko
ninapoishi, na duka hilo limeshakamiliko kwa asilimia kubwa hivyo
natarajia lianze kutoa huduma mwakani, hili gari kwangu naona kama
baraka toka kwa Mwenyezi Mungu na mwanzo mzuri wa biashara yangu kwani
limekuja wakati muwafaka, Asante sana Samsung kwa kuwajali wateja wenu
haikuwa raisi kuamini mara pale tu nilipopokea simu lakini sasa naamini
kweli nimeshinda gari hili” alisema Bw Juma mara baada ya kukabidhiwa
garii lake.
Akizungumzia
jinsi alivyoshiriki kwenye promosheni hiyo Bw. Juma alisema kwamba
“Nilinunua simu ya Samsung na kisha kujisajili katika mfumo wao maalum
wa dhamana ambapo nilitambulishwa kwamba simu yangu ni halisi na
imesajiliwa na Samsung Tanzania, hilo lilinipa furaha kwa kununua simu
halisi lakini sikuwa najua kama nimeingia kwenye droo ya Pambika na
Samsung, hivyo hata nilipopigiwa simu hii haikuwa rahisi mara moja
kuamini nilichokuwa nikisikia toka upande wa pili”.
Akikabidhi
gari hilo mara baada ya kuwasili dukani kwa mshindi huko Tabata Segerea
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw Sylvester Manyara
alisema kwamba promosheni hiyo aliandaliwa maalum kwa ajili ya kutoa
elimu kwa Watanzania juu ya athari zitokanazo na manunuzi ya bidhaa feki
zilizoenea sokoni lakini pia kuhamasisha wananchi kununua bidhaa halisi
na kuzisajili kwa mawakala walioidhinishwa.
“Napenda
kuwashukuru wale wote walioshiriki katika promosheni hii, kupitia
promosheni ya Pambika na Samsung kumekuwa na ongezeko la zaidi ya
asilimia 30 la wateja walionunua bidhaa halisi na kujisajili hivyo ni
ishara njema kwamba kama wadau kushirikiana na mamlaka husika nchini
Tanzania tukiungana pamoja kupambana na bidhaa feki basi tunaweza
fanikiwa vita hiyo kwa asilimia kubwa. Ni matumaini yetu kwamba bado
manunuzi ya bidhaa halisi yataenedelea hata mara baada ya kuisha kwa
promosheni hii” alisema Bw. Manyara
Jumla
ya washindi 90 wamepatikana katika kipindi cha wiki sita toka kuanza
kwa promosheni ambapo katika droo za kila wiki walikuwa wanatoka
washindi 15 waliokuwa wakijishindia bidhaa mbalimbali za kila wiki huku
zawadi kubwa ikiwa ni gari jipya aina ya Mitsubishi Double Cabin
iliyokuwa imesheheni bidhaa mbalimbali toka Samsung.
NA MO BLOG
0 comments:
Post a Comment