Kocha
wa Mbeya City, Juma Mwambusi (katikati), akiwapatia maelekezo vijana
wake Hassan Mwasapili (kushoto) na Peter Richard (kulia)
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
KLABU
ya Mbeya City Kwa mara ya kwanza inakutana na timu kutoka nje ya
Tanzania ambazo zitashiriki michuano ya Mapinduzi inayotarajia kuanza
kushika kasi januari mosi mwakani katika Uwanja wa Amaan mjini Unguja na
Gombani kisiwani Pemba.
Klabu
hii imepanda ligi kuu msimu huu na tayari imeshaonesha kiwango cha juu
kwa kuziwekea ngumu timu kubwa za Simba, Yanga na Azam fc , na kumaliza
ngwe ya kwanza ligi kuu ikijikusanyia pointi 27 katika nafasi ya tatu
bila kupoteza mchezo wowote.
Mbeya City wanakwenda Zanzibar huku wakijua wazi kuwa wanakwenda kukabiliana na changamoto kubwa tatu.
Moja; wanashiriki kwa mara ya kwanza michuano hii mikubwa tangu kuanzishwa kwao.
Pili;
wanakwenda kukutana kwa mara ya kwanza na timu za Kenya , Uganda zenye
wachezaji wanaocheza mazingira tofauti na ligi kuu Tanzania bara.
Tatu; wanakwenda kukutana na timu za visiwani Zanzibar kwa mara ya kwanza.
Ukiangalia mambo haya matatu, utagundua kuwa Mbeya City ni wageni wa kila kitu kuelekea mashindano haya.
Lakini
ni nafasi yao kuoenesha ubora wao kama walivyofanya ligi kuu. Pia
itasaidia kupima uwezo wa wachezaji wao mbele ya timu ngeni kabisa
machoni kwao.
Itakuwa changamoto mpya kwa wachezaji wa Mbeya City, ambapo wengi wao ni vijana wanaochipukia katika soka la ushindani.
Ukitazamana
timu zenye majina makubwa mfano URA, Tusker, AFC Leopard , KCC, Simba,
Yanga, na Azam fc, Mbeya City imekutana na timu tatu tu yaani Simba,
Yanga na Azam fc kwenye michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Na
ndipo kocha mkuu wa klabu hiyo, Juma Mwambusi anakiri wazi kuwa michuano
hii ni migumu kwake, hivyo ameichukulia uzito wa hali ya juu.
Kikosi cha Klabu ya Mbeya City
Ili
kukabiliana na changamoto mpya, Mwambusi alisema atatumia kikosi cha
kwanza kupima uwezo wa wachezaji wake mbele ya wachezaji wa kimataifa
kwa lengo la kujiridhisha kabla ya kuanza mzunguko wa pili ligi kuu.
“Tunaenda
kushiriki kwa mara ya kwanza. Vitu vingi sisi ni wageni, lakini naamini
maandalizi yetu yatatupatia mafanikio. Mwenyezi Mungu akitupa uzima,
tutawasili Zanzibar desemba 31”. Alisema Mwambusi.
Mwambusi
alisema uwepo wa Simba sc, Yanga na Azam fc sio tatizo kwao kwani
afadhali wameshakutana ligi kuu, lakini changamoto kubwa ni timu ngeni
kutoka Kenya na Uganda .
Hata
hivyo, Mwambusi aliongeza kuwa timu za Tanzania bara zimeongeza
wachezaji wapya , hivyo wataongeza kasi tofauti na mzunguko wa kwanza
wa ligi kuu.
Yanga wameongeza nguvu kwa kumsajili Kipa, Juma Kaseja, Kiungo, Hassan Dilunga , na mshambuliaji , Mganda Emmanuel Okwi
Michuano
iliyopita, Yanga haikushiriki kwani kwa wakati ule ilikuwa na ziara
nchini Uturuki (Barani Ulaya) kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu
ambao waliishia kutwaa ubingwa na kuivua Simba sc.
Kwa
upande wa Simba, nao wameongeza wachezaji wapya katika dirisha dogo
ambao ni Uhuru Selemani, Ivo Mapunda, Ali Badru, Awadh Juma, Donald
Mosoti na Yaw Berko.
Azam
fc wao hawakuona haja ya kuongeza wachezaji wengi, lakini wamemsajili
mshambuliaji mmoja kutoka nchini Ivory Coast, Mouhamed Kone, hivyo
kuongeza kasi zaidi katika safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Kipre
Tchetche pamoja na nahodha John Bocco, `Adebayor`.
Mabadiliko
hayo katika vikosi vya timu hizi za Bara yanampa shida kocha Juma
Mwambusi kwani ni wachezaji mahiri, lakini ametamba kuonesha kandanda
bora kama kawaida yao.
Timu
za Azam fc, Simba sc na Yanga zimeshatangaza kushuka na vikosi vyao vya
kwanza “full nondo” kwa lengo la kupima uwezo wa wanandinga wao.
Tofauti
na Simba, Mbeya City ambazo malengo yao ya kushiriki mashindano hayo ni
kuandaa vikosi kwa ajili ya ligi kuu, klabu za Yanga , KMKM na Azam fc
zitayatumia mashindano haya kuandaa vikosi vyao kwa ajili ya michuano ya
ligi kuu na kimataifa barani Afrika.
0 comments:
Post a Comment