Kilio cha furaha kwa Moureen Julius.
Wow.....!!!...Hongera Mwanangu.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akikabidhi kitita cha Shilingi Milioni tano za Kitanzania kwa Supa
Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12).
Wanaoshuhudia tukio hilo ni baba mzazi wa Moureen pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji wa shindano hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko, akiwa ameongozana na Supa
Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12) huku
nyuma yao wakiwa na ulinzi mkali kuelekea kuzungumza na waandishi wa
habari.
Supa
Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12),
akifanya mahojiano na waandishi wa habari. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer.
Kijana
Salum Nyangumwe (17) mshindi wa pili aliyeimba wimbo wa My Number One
wa Msanii Nasib Abdul a.k.a Diamond wakati wa fainali za kusaka kipaji
cha SUPA STAA wa watoto na vijana! la ”MO Kids Got Talent 2013"
lililofanyika mwishoni mwa Juma kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari
Beach jijini Dar es Salaam.
Na.Mwandishi wetu.
Mtoto
Moureen Julius(12), amejinyakulia kitita cha shilingi Milioni tano
katika fainali za Shindano la “MO KIDS GOT TALENT 2013” lililofanyika
kwenye hoteli ya Ledger Plaza Bahari beach lililoanza tarehe 25 hadi
tarehe 28 mwezi huu ambapo fainali zilifanyika.
Shindano
hilo lilijumuisha watoto zaidi ya mia mbili ambapo kila mmoja
alijipatia nafasi ya kuonesha kipaji chake vikiwemo kuogelea, kuimba,
kucheza, karate na vingine vingi.
Watoto
15 walichuana katika nusu fainali na kuchujwa hadi kufikia watoto
watano na mwisho wa siku kupatikana SUPA STAA Moureen Julius
aliyewafunika wenzake kwa kipaji alichonacho.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza
aliyejinyakulia kitita cha sh.millioni tano, Mtoto Moureen Julius
alisema pesa hizo alizoshinda atazitumia kwa kulipia ada na vifaa
vingine vya shule.
Shindano
hili la "MO KIDS GOT TALENT 2013" liliandaliwa na Frost Africa na
kudhaminiwa na Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL) Group.
Supa
Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12)
akionyesha kipaji chake cha kucheza kwenye fainali za shindano hilo.
Pichani
juu na chini washiriki wa shindano la "MO Kids Got Talent 2013"
wakiendelea kuonyesha vipaji vyao wakati wa fainali za shindano hilo.
Mtoto mwenye kipaji cha kuimba na kucheza.
Jaji
Hidaya Njaidi akitoa maoni yake kwa washiriki (hawapo pichani)
waliokuwa wakichuana kuwani Shilingi Milioni 5 za Kitanzania
zilizotolewa zawadi na Kampuni ya MeTL Group.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji wa mashindano hayo na Meneja
Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (kulia) wakifuatilia
kwa umakini mashindano hayo yaliyomalizika mwishoni mwa Juma.
Jaji Mkuu wa shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Salma Mziray akitoa maoni yake kwa washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora.
Pichani
Juu na chini ni baadhi ya washiriki waliofanikiw kuingia tano bora
wakionyesha manjonjo yao kwa mara nyingine tena kabla ya kutajwa mshindi
wa shilingi Milioni tano kutoka Kampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Ltd. MeTL Group lilifanyika mwishoni mwa Juma kwenye Hoteli ya
Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar.
Jaji
Kiongozi wa shindano la "MO Kids Got Talent 2013" akiteta jambo na
Raisi wa wanafunzi, Allan Lucky a.k.a SKONGA kabla ya kutangaza mshindi.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer na Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko wakionekana kufurahishwa na vipaji vya watoto hao.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko, akitoa nasaha kwa
washiriki walioingia tano bora ambapo amewata wazazi kuhakikisha
wanaendeleza vipaji vya watoto.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akiwapongeza vijana walioingia tano bora.
Tano Bora wakiwa na matumbo joto.
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akitoa nasaha zake ambapo
amesema mashindano haya yatakuwa yakifanyika kila mwaka nchini lengo ni
kuibua vipaji vya watoto na vijana.
Mshindi
wa tano Gloria Collin (10), akipokea maboksi ya zawadi zilizotolewa na
kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) kutoka kwa Afisa
Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji
wa mashindano hayo.
Mshindi wa nne Lisa Deogratius (17) naye alipkeza zawadi mbalimbali kutoka kampuni ya MeTL.
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akiwausia washiriki ambao
mmoja kati ya hao ataibuka mshindi wa kitita cha shilingi milioni tano
kutoka MeTL Group.
Jaji
Kiongozi wa shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Salma Mziray akitoa
shukrani kwa kampuni ya MeTL kwa kuweza kuibua vipaji vya watoto na
vijana.
Na mshindi niiiiiiiiiiiii.....!!!! Raisi wa wanafunzi, Allan Lucky a.k.a SKONGA akitangaza mshindi.
Mtoto Moureen Julius (12) akilia kwa furaha baada ya kuibuka mshindi.
Sehemu
ya watoto, wazazi/walezi waliohudhuria fainali za shindano la "MO Kids
Got Talent 2013" lililofanyika mwishoni mwa juma kwenye hoteli ya Ledger
Plaza Bahari Beach.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment