Waumini
wa Kanisa la Anglikana Ilela Ludewa wakimshangilia mbunge wao
Deo Filikunjombe wakati akitolea ufafanuzi wa misaada anayoitoa
kanisani hapo wakati wa ibada ya Krismas
Mmoja kati ya waumini wa kanisa hilo akishukuru kwa kulala chini wakati mbunge wao akitoa misada yake
Mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wa pili kulia akikabidhi
msaada wa marumaru seti 100 kwa mchungaji wa kanisa la Anglikana
mtaa wa Ilele Ludewa mchungaji Canon Ngoye
Wananchi
na waumini wa kanisa la Anglikana mtaa wa Ilela Ludewa
wakimuwekea mikono ya baraka mbunge Deo Filikujombe baada ya kukabidhi
misaada kanisan i hapo
Waumini
wa kanisa la Anglikana mtaa wa Ilela Ludewa akifurahi pamoja na mke
wa mbunge Deo Filikunjombe Bi Habiba Filikujombe mwenye nguo nyekundu
kati
Waumini wa kanisa hilo wakimshangilia mbunge wao
Mmoja
kati ya waumini wa kanisa hilo akimfuta jasho mbunge Deo
Filikunjombe kama ahsante kwa kuwajali wapiga kura wake
Mbunge Filikunjombe akitoa neno kwa wapiga kura wake kanisani hapo
Mbunge Deo Filikunjombe akitoa neno
Mkuu
wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha kulia akiwa na mbunge wa jimbo la
Ludewa Deo Filikunjombe kati na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa
Bw Kolimba wakati wa ibada ya Krismas jana
Mchungaji wa kanisa la Anglikana mtaa wa Ilela Canon Ngoye akikabidhiwa kinada na mbunge Deo Filikunjombe
Mchungaji Ngoye akikabidhiwa saruji mifuko 20 kutoka kwa mbunge Deo Filikunjombe wakati wa ibada ya Krismas
**********
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe amekabidhi msaada wa vitu mbali mbali kwa uongozi wa kanisa la Angilikana mtaa wa Ilela wilaya ya Ludewa kama sehemu ya kutimiza ahadi yake kwa waumini wa kanisa hilo.
Mbunge huyo alitimiza ahadi hiyo wakati wa idaba ya Krismas ambapo alijumuika na familia yake kusali pamoja na kula na wagonjwa wa kituo cha afya Manda kama sehemu ya mwendelezo wa ushirikiano wake na wapiga kura wake .
Alisema kuwa kila sikukuu amekuwa na utamaduni wa kuzunguka katika moja kati ya kanisa la jimboni kwake na kula sikuku ya wagonjwa pamoja na kusali na waumini wa madhehebu mbali mbali jimboni humo lengo likiwa ni kuhimiza shughuli za maendeleo jimboni .
Hata hivyo akizungumzia mambo mbali mbali ya kimaendeleo katika jimbo hilo alisema kuwa ameendelea kuisukuma serikali kutatua kero za wananchi wa jimbo la Ludewa ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu ikiwemo barabara , afya ,elimu ,maji na kero nyingine ambazo wananchi wamekuwa wakihitahi ufumbuzi wake.
Filikunjombe alisema kuwa kuhusu kilichotokea bungeni kwa mawaziri wanne kuenguliwa uteuzi wao yeye kama mbunge anaona walichokipata mawaziri hao ni haki yao na kamwe hataacha kuwapigania wananchi wake wa Ludewa kwa kuwanyoshea vidole mawaziri wasiowajibika katika nafasi zao.
Kwani alisema mbali ya mawaziri hao bado wapo viongozi mbali mbali wa serikali ambao wamekuwa wakifanya kazi kimazoea kwa kushindwa kuwajibika katika nafasi zao na kusababisha kero kwa wananchi na hata kuichukia serikali yao iliyopo madarakani.
Pia alimpongeza Rais Dr Jakaya Kikwete kwa kutimiza kwa wakati ahadi yake ya gari la wagonjwa katika Hospital ya wilaya ya Ludewa ahadi ambayo aliitoa wakati wa ziara yake mkoani Njombe mapema mwaka huu.
Kwani alisema kuwa utekelezaji wa ahadi za Rais kwa wananchi wa jimbo la Ludewa zinaendelea kuwavutia wananchi wa jimbo hilo na kuwataka wananchi wa Ludewa kuwa wavimilivu na kuendelea kuwa na imani na viongozi wao na kuacha kulalamika pale ahadi husika inapochelewa kutolewa .
Miongoni wa misaada iliyotolewa na mbunge huyo ni pamoja na marumaru seti 100, mifuko 20 ya saruji ,kinada cha kisasa kwa ajili ya kanisa na sare seti mbili za kwaya
kanisani hapo.
CHANZO: MICHUZI MATUKIO
0 comments:
Post a Comment