SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, October 26, 2013

Waandishi wa habari walifanya ziara Azam Tv jijini Dar Jana

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media,Rhys Torrington akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari waliopata fursa ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo juu ya uanzishwaji wa Televisheni yao ya Azam TV yenye muonekano wa kisasa zaidi na yenye lengo la kukuza michezo mbali mbali hapa nchini,zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media,Rhys Torrington akionyesha King'amuzi cha Azam TV kwa baadhi ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) waliopata fursa ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo,zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi wa Wakuu wa Idara mbali mbali za Kampuni ya Azam Media wakimsikiliza Mkurugenzi wao.
 Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Azam Media,Loth Mziray (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya Waandishi wa habari waliopata fursa ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo,zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Azam Media (Kitengo cha huduma kwa Wateja) wakiwajibika.
Meneja Uzalishaji na Ufundi wa Kampuni ya Azam Media,Mehboob Aladdad akionyesha moja ya mixer za sauti zilizopo ndani OB Van ya Azam TV ambayo ni ya kisasa na yenye vigezo vya kimataifa,wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo,zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam jana.
Sehemu ya vifaa vya kuchanganyia picha kwenye OB Van ya Azam TV.
Wazee wa Kazi ndani ya OB Van la Azam Tv,toka kulia ni Meneja Uzalishaji na Ufundi wa Kampuni ya Azam Media,Mehboob Aladdad,Meneja wa Azam FM na Matukio ya Moja kwa Moja,Yahya Mohamed pamoja na Fundi Mitambo wa OB Van hiyo,Saleh Mansoor (alieketi) wakifatilia moja ya kazi zao.
OB Van ya Azam TV ikiwa imetukia tayari kwa lolote.
NA MICHUZI MATUKIO BLOG

0 comments:

Post a Comment