

Vitendo vya ubakaji vimeendelea
kuumiza akili za wapigania haki na ustawi wa wanawake nchini Tanzania
kwa muda mrefu sasa. Miongoni mwa kesi hizi zimehusisha wasichana wadogo
wenye malengo makubwa katika maisha yao, lakini kutokana na mfumo
uliopo, jamii hushindwa kutoa msaada kwa wahanga wa matukio hayo ili
wafanikishe malengo yao.
Emma Roberts ni binti mwanafunzi
aliyekumbwa na mkasa wa kufukuzwa shule kutokana na ujauzito alioupata
baada ya kubakwa. Kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na
East Africa Television kila Jumanne saa tatu usiku, binti Emma anaelezea
tamaa yake ya kufanya mtihani mwezi Novemba, kwa kuwa anaamini kuwa
elimu itamsaidia yeye na mwanaye ambaye atalelewa bila kuwa na baba.
Kitendo cha kufukuzwa shule kwa tukio kama hili kumemuathiri kwa kiasi
kikubwa, na sasa ana hofu ya kutimia kwa malengo yake hapo baadae.
Tembelea www.wanawakelivetv.com kwa taarifa zaidi, picha na video.
Kumnyima fursa hiyo ya kuendeleza
elimu yake ni kutengeneza taifa lenye wanawake wasio elimu na masikini.
Kitendo kilichomkuta Emma, kinaweza kuwakuta wasichana wengi nchini
Tanzania. Kuna wale waliojitokeza hadharani, lakini vipi kuhusu wale
walioamua kukaa kimya?
SOURCE: www.wanawakelivetv.com
Maelezo ya picha;
-wanawakelive1 - Joyce Kiria akiwa amembeba mtoto wa Emma
-wanawakelive2 - Joyce Kiria akizungumza na Emma
0 comments:
Post a Comment