Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongoza kikao kati ya balozi
wa Tanzania nchini Congo DRC Balozi Anthony Cheche aliyefika ofisini
kwake kwa lengo la kujitambulisha na kujadili mambo mbalimbali ya
kimahusiano kati ya nchi hizo mbili. Mkuu huyo wa Mkoa alimuomba balozi
Cheche kunadi fursa za uwekezaji zinazopatikana Mkoani Rukwa pamoja na
kuunganisha nguvu ya nchi hizi mbili katika kuwekeza kwenye usafiri wa
majini katika Ziwa Tanganyika. Akizungumzia kuhusu wahamiaji haramu
amesema ni bora kujenga ushirikiano mzuri wa kibiashara kwa nchi zote
mbili ambapo taratibu maalum zitafuatwa kwa wananchi na wafanyabiashara
kuingia na kutoka.
Balozi
Anthony Cheche anayoiwakilisha Tanzania nchini DRC akizungumza Ofisini
kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa leo alipoonana na uongozi wa Mkoa kwa lengo la
kujitambulisha na kujadili mambo kadhaa ya mahusiano kati ya Tanzania
na Congo DRC. Ameiomba Serikali ya Tanzania kuangalia upya vizuizi vya
njiani kwa wafanyabiashara wa nje ikiwemo DRC hususani uwepo wa mizani
nyingi barabarani na badala yake ziwepo chache na ziwe mbali kidogo na
barabara kuepusha usumbufu kwa wasafiri wengine na wafanyabiashara.
Balozi Anthony Cheche akizungumza katika kikao hicho.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimuonyesha Balozi cheche
toleo maalum katika gazeti la Daily News linaloelezea fursa mbalimbali
za uwekezaji zinazopatikana Mkoani Rukwa kwa ajili ya kuzinadi kwa
wawekezaji nchini Congo DRC.
Baadhi
ya wakuu wa idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa wakiteta jambo
katika kikao hicho, Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na
Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi
Idara ya Mipango Ndugu David Kilonzo na Kaimu Katibu Tawala Idar a ya
Uchumi na Uwezeshaji Ndugu Respitch Maengo.
Picha ya pamoja.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiagana na Balozi Anthony
Cheche baada kuonana na uongozi wa Mkoa huo mapema leo katika jengo la
ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Rukwa
0 comments:
Post a Comment