SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 3, 2013

Mwili wa Marehemu Mzee Felician Makwaia wasafirishwa Jana kwenda Bukoba kwa Mazishi


 Picha ya Marehemu Mzee Felician M. Makwaia enzi za uhai wake.

 Watoto wa Marehemi Mzee Felician Makwaia,Christopher Makwaia ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group (wa kwanza kulia,waliovalia fulana zenye picha),Frank Makwaia,Robert Makwaia pamoja na Elizabeth Makwaia wakiwa wamesimama pembeni ya Jeneza lenye mwili wa Marehem baba yao.Mwili wa Mzee Makwaia umesafirishwa Jana kwenda kijijini kwake huko Bukoba mkoani Kagera kwa mazishi
 Mjane wa Marehemu Mzee Makwaia,Mama Makwaia (wa pili kulia).
 Katekist wa Kanisa Katoliki Mwenge,akiongoza ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Mzee Felician Makwaia.
 Neno la Mungu likisomwa.
 Wasifu wa Marehemu Ukisomwa.
 Waombolezaji waliofika kuaga mwili wa Marehemu Mzee Felician Makwaia nyumbani kwa Familia Sinza Mori,jijini Dar es Salaam leo.Mwili wa Mzee Makwaia umesafirishwa leo kwenye Bukoba kwa mazishi. 
 Watoto wa Marehemu,kutoka kulia ni Frank Makwaia,Robert pamoja na Christopher Makwaia ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group.
 Waombolezaji wakiacha mwili.
 Mtoto wa Mwisho wa Marehemu Mzee Makwaia,Christopher Makwaia ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Michuzi Media Group akiuaga mwili wa Baba yake.
 Mjane wa Marehemu akiaga.
 Safari imeanza.
NA ISSA MICHUZI

0 comments:

Post a Comment