SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, October 22, 2012

Mh. Lowassa Azindua Maonyesho Ya Biasara Za Wajasiliamali Wa VICOBA Jijini Dar


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania, Aldo Mfinde wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar tayari kwa Uzinduzi rasmi wa maonyesho ya VICOBA Tanzania.Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde akizungumza machache wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.wa Tatu kulia ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.Wengine ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga (pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akimpongeza Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde mara baada ya kumaliza kuitambulisha Kamati ya VICOBA Tanzania iliokuwepo viwanjani hapo.
Burudani ya Ngoma za Asili.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda akisoma Risala ya Chama chao hicho mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda (kushoto) akikabidhi Risala hiyo kwa Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba akisalimia Wanachama wa VICOBA Tanzania.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuzungumza na Wanachama wa VICOBA.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake mbele ya wanachama wa VICOBA Tanzania wakati hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Katika Hobuba yake,Mh. Lowassa aliwapongeza wana VICOBA kwa kuweza kujiajiri,kwani tatizo la ajira nchini bado ni tatizo kubwa na ni bomu linaweza kulipuka wakati wowote.Maonyesho hayo yataendelea mpaka jumamosi ijayo Oktoba 27.

0 comments:

Post a Comment