SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, August 4, 2012

SHULE YA MWANAKWEREKWE C YAPATA UFADHILI TOKA WATU WA CHINA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza  Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ujenzi ya Fujian Group Company ya China Bw. Xiong Kaihua akitowa maelezo ya ramani ya ujenzi wa skuli mpya ya Msingi ya Mwanakwerekwe C 
Skuli hiyo inajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China ikiwa ya pili ikitanguliwa na ile ya Kijichi iliyoko Wilaya ya Magharibi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua ujenzi wa Skuli mpya ya Msingi ya Mwanakwerekwe C unaogharamiwa na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa Chinankwa gharama ya Dola za Kimarekani Milioni 1.6.Kushoto ni Balozi mdogo wa China aliyepo Zanzibar Bi.Chen Qiman.
Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Bi Chen Qiman akimkabidhi madeski 480 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi yaliyotolewa na Serikali ya Jimbo la Sichuani  China yenye  gharama ya Yuan za Kichina Milioni Moja.

0 comments:

Post a Comment