SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, June 12, 2012

Rais Jakaya Kikwete Awaapisha Mabalozi Wapya Kumi Ikulu Jijinin Dar es Salaam na amwapisha Mkuu Mpya Wa Mkoa wa Ruvuma

 Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Balozi Bertha Semu Somi Ikulu Jijini Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete Akimwapisha Balozi Dora Mmari Msechu Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz ikulu jijini Dar es Salaam
Rais jakaya kikwete akimwapisha  Balozi Dora Mmari Msechu Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Jana amewaapisha mabalozi wapya kumi ambao wataongoza idara na kurugenzi mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pichani Rais akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kutoka kushoto walisimama mstari wa mbele ni Balozi Bertha Semu Somi,Balozi Hassan Simba Yahya, Balozi Vincent Joel Thomas Kibwana,Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz,Balozi Irene Mkwawa Kasyanju na Balozi Dora Mmari Msechu.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi Silima Kombo Haji,Balozi Celestine Joseph Mushy, Balozi Mbelwa Brighton Kairuki na Balozi Ramadhan Muombwa Haji.
Picha na Freddy Maro-IKULU
****

 Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Ruvuma Bwana Hassan Mpapi Bendeyeko akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI Dkt.Aldin Mutembei akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitabu cha kwanza cha fasihi simulizi ya jamii ya Wakwere ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa Idara ya historia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Kapepwa Tambila. Dkt.Mutembei ambaye pia ni mchapishaji na msimamizi wa tafiti za Tamaduni lugha na fasihi za makabila ya Tanzania alikabidhi pia kamusi Asisi ya Kiingereza-Kiswahili na Kiarabu.
Picha na Freddy Maro-IKULU

0 comments:

Post a Comment