SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 31, 2012

SERIKALI YACHANGIA MILIONI 10 KAMA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU KANUMBA

Tunafarijika sana sisi wasanii na serikali yetu ya sasa hatuna cha kuwapa zaidi ya shukrani zetu za dhati kwenu kwa kipaumbele mnachotupatia kwa sasa hii haijawahi kutokea katika serikali zote zilizopita tunakushukuru sana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kututhamini sisi wasanii wa Tanzania, kwanini nasema hivi leo.., serikali yetu ya Tanzania imetoa milioni kumi kwa famila ya marehemu Steven Kanumba kama rambirambi ya serikali yetu. Familia ya The Great na sisi wasanii wote Bongo Movie tunasema tunawashukuru sana..

Naibu Waziri wa utamaduni na michezo Mhe, Amos Makalla akiwa anawasili nyumbani kwa marehemu Kanumba kwa ajili ya kutoa rambirambi hiyo sisi wasanii tunasemaje Mhe.Amosi Makala ni chaguo sahihi katika wizara aliyopewa tunampenda sana maana anajali sana wasanii
Mh; Amos Makalla akisalimiana na Mama mzazi wa The Great

Mheshimiwa akiwa makini kufuatiliia ratiba zinazoendelea..
Mama wa marehemu (Mama Frola) akiwa na majonzi akisubiri kinachoendelea.
CHANZO: BOFYA HAPA

0 comments:

Post a Comment