SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, January 16, 2012

RAIS KIKWETE KATIKA MSIBA WA MAREHEMU REGIA MTEMA TABATA JIJINI DAR JANA

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Freeman Mbowe katika msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Mh Regia Mtema jana nyumbani kwa marehemu, Tabata jijini Dar es Salaam ambako Waziri Mkuu, Mh Mizengo Pinda, Spika Anne Makinda na waheshimiwa Mbalimbali walikuwepo.
Rais Jakaya Kikwete akitoa mkono wa pole kwa waombolezaji katika msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Mh Regia Mtema jana nyumbani kwa marehemu, Tabata jijini Dar es Salaam ambako Waziri Mkuu, Mh Mizengo Pinda, Spika Anne Makinda na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Freeman Mbowe walikuwapo, wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Tundu Pinda.
Rais Jakaya Kikwete akiagana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) muda mfupi baada ya kuwasili na kujiunga na waombolezaji katika msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Mh Regia Mtema jana nyumbani kwa marehemu, Tabata jijini Dar es Salaam ambako Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda, Spika Anne Makinda (kushoto) na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Freeman Mbowe walikuwapo.
Rais Jakaya Kikwete akijiunga na waombolezaji katika msiba wa Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA), Mh Regia Mtema jana nyumbani kwa marehemu, Tabata jijini Dar es Salaam ambako Waziri Mkuu, Mh Mizengo Pinda, Spika Anne Makinda na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Freeman Mbowe (wa tatu kushoto) walikuwapo.
PICHA ZOTE NA IKULU
Source: Global Publishers.

0 comments:

Post a Comment