SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, January 11, 2012

MZEE KIPARA WA KAOLE AFARIKI


MSANII mkongwe katika tasnia ya Maigizo/Filamu hapa nchini, almaarufu kwa jina la kisanii Mzee Fundi Said, aliyevuma katika fani hiyo tangu akishiriki uigizaji vipindi vya Radio Tanzania hadi kundi la Kaole, amefariki leo asubuhi majira ya saa 3:30 huko Kigogo Mbuyuni-Kinondoni jijini dar.
Hali ya msanii huyo ilianza kuwa ya utata miaka ya karibuni akisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kimwili ambapo jana hali yake ilikuwa mbaya wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika makazi yake katika nyumba inayomilikiwa na kundi la Kaole.
Mtandao huu utawaletea habari zaidi za tukio hilo pindi zitakapopatikana.
24 SEVEN 365 inawapa pole ndugu na jamaa wa familia ya mzee Kipara, bila kuwasahau wasanii na wadau wote kwani wa Tasnia ya Filamu hili ni pigo kubwa kwani Mzee Kipara alikuwa ni msanii nguli, baba yetu na ni kiongozi kwetu, na wasanii wengi wamefika hapa kutokana na kufuata nyayo zake.

HISTORIA YAKE KWA UFUPI:
Mzee kipara ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1922,huko Bongoni mkoani Tabora,alikuwa kisumbuliwa na matatizo ya miguu kukosa nguvu,alikuwa hawezi kusimama mwenyewe,sambamba na umri nao huenda ulichangia kwa maradhi hayo na mengineyo,hali iliyokuwa ikimlazimu kutumia muda mwingi kitandani,wakati mwingine alishindwa kutoka nje mpaka watu watokee kumtoa nje ili kuota jua ama kupunga upepo.

Mzeee Kipara alianza sanaa mnamo mwaka 1964 kwa kufanya kazi za mitaani na baadaye akachukuliwa na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) sasa TBC Taifa. Akiwa na kituo hicho, aliigiza katika michezo mingi na nafasi zake kubwa zilikuwa zile zenye kuonesha utemi, wengi huita ukorofi. Mnamo Mwaka 1999, akiwa na wasanii wenzake akina Zena Dilip, Rasia Makuka, marehemu Rajab Hatia ‘Mzee Pwagu’ na Mama Haambiliki walijiunga katika Kundi la Kaole ambalo lilikuwa likirusha maigizo yake katika Runinga ya ITV.

Taarifa zaidi za msiba huo na mazishi tutafahamishana zaidi hapo baadaye kidogo.
 Mungu ailaze mahali pema roho ya mzee wetu, Ameen
PICHA NA GLADNESS MALLYA, GPL

0 comments:

Post a Comment