SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, December 22, 2011

Maafa Ya Mvua Jijini Dar es Salaam!!

Hii ndio hali halisi kwa wakazi wa eneo la Jangwani leo mara baada ya mvua kubwa kuendelea kunyesha jijini Dar es Salaam leo na kuyafanya makazi ya wakazi wa eneo hili kuwa namna hii kama zinavyoonyesha picha hizi.

Mbunge wa Mafia, mkoani Pwani, Abdulkarim Shah, akiwa kwenye boti aliyoikodi kwa ajili kusaidia kuokoa wananchi wa maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam leo,  akitoa maelekezo kwa nahodha ni sehemu gani ya kupita wakati alipokuwa akishiriki katika kuwaokoa baadhi ya wananchi  waliokumbwa na mafuriko.


Mmoja wa wakazi wa eneo hilo akijaribu kupita kwenye maji hayo ili afike barabari kwa kujiokoa na mafuriko hayo.

Nyumba zote zimezungukwa na maji huku mengine yakiwa yamejaa ndani ya nyumba hizo.

Kwa mbaali anaonekana mmoja wa wakazi wa eneo hilo akiwa kapanda juu ya paa la nyumba yake ili kujirusuru na mafuriko hayo ambayo yameenea katika kila kona ya eneo hilo la Jangwani jana.

Mmoja wa wakazi wa eneo la Jangwani Jijini Dar akiwa amekaa juu ya godoro mara baada ya kuokolewa na waokoaji waliofika katika eneo hilojana.

Yaani ni kama bahari ilikuwa imeamia hapa maana maji yalienea kila kona.

Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia wakijaribu kuwazua watu waliokuwa wakiitumia barabara ya morogoro rodi kutokana na kujaa maji kwa barabara hiyo jana.

Wakazi wa Jangwani wakiwa juu ya mapaa yao wakisubiri kupatiwa msaada.

Askari wa Jeshi la Wananchi wakiwa na mtumbwi wakisaidia kuwaokoa wananchi ambao wamekubwa na Mafuriko hayo katika eneo la Jangwani jijini Dar.

Yaani hali ni mbaya sana kwa wakazi wa eneo hili maana mambo ni kama yanavyoonekana pichani hapa.

Waokoaji wakiwa katika kazi

Wengi walilazimika kutembea kwa miguu leo kwani hakuku na gari iliyokuwa ikiruhusiwa kupita katika eneo la Jangwani Jana.

Wananchi wakisaidiana kushusha mtumbwi katika eneo la jangwani tayari kwa kazi ya kuokoa waliokwama kwenye mafuriko hayo.

Gari la wagonjwa likipita huku na kule kuona kama kuna yeyote anaehitaji msaada.
CHANZO: MICHUZI MATUKIO

1 comments:

Anonymous said...

Mdau wa 24 SEVEN 365 wa 6000
Poleni mliofikwa na janga hili Mungu awape subira na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu kwa kuwapoteza ndugu zetu walifariki na mafuriko haya, mliopo mahospitali mungu awape afya mpone. Hongera sana Mbunge wa Mafia, mkoani Pwani, Abdulkarim Shah, kukodi boti kwa ajili kusaidia kuokoa wananchi wa maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam. Huu ndio tunaosema ni uzalendo Upendo na Moyo wa Huruma. Jamani kujitolea ni moyo na utajiri tuwasaidie ndugu zetu hali sio nzuri, asante.

Post a Comment