Ankal akielezea mambo ya libeneke kwenye ukumbi wa mkutano wa White House baada ya waandishi wa White House na wa nchi mbalimbali kumuomba aelezee jinsi tasnia ya habari ilivyo Bongo kwa hivi sasa, hususan swala la kuibuka kwa 'vikombe' karibu kila kona ya nchi.Ankal aliwaambia kwamba ni kweli kumezuka watoa dozi sehemu kadhaa lakini hadi sasa Babu wa Loliondo ndiye anayetamba kuliko wengineo wote.Ankal alipata wakati mgumu sana kuelezea ni namna gani kikombe kimeshika hatamu Bongo.
Ankal ameiambia Globu ya Jamii usiku huu kwamba wadau wake wala wasiwe na hofu kwani libeneke litaendelea kama kawa kwani kaacha timu kubwa ya kuendeleza libeneke na wakati huo huo atakuwa akileta mambo moja kwa moja toka sebuleni kwa Obama.
VOA wamekuwa wakimzengea sana Ankal ili akafanye kazi kwenye idhaa hiyo ya Kiswahili upande wa habari za mtandaoni. Akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Juma Nkamia, ambaye sasa ni Mbunge wa Kondoa.
Ankal akiwa ofisi za masuala ya nje ya Marekani (State Department) ambako ndiko ziliko ofisi za Bi.Hilarly Clinton.Kazi yake ya kuripoti habari za Ikulu ya Marekani huhusika na ofisi hii pia.Ameiambia Globu ya Jamii kwamba anamshukuru Mungu kwa 'kudakwa' na VOA na hivi sasa anajiandaa kupigana vikumbo na wanahabari wa dunia.
BOFYA HAPA

0 comments:
Post a Comment