SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, July 30, 2010


mama Salma Kikwete Akiunguruma....
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akichangia akichangia wakati wa kikao cha wake wa marais na wakuu wa nchi za Afrika kilichofanyika Kampala nchi Uganda juzi.Picha na John Lukuwi


Iraq yazidi kugubikwa na machafuko, kuundwa serikali bado ni kitendawili


Watu wasiopungua 21 wamepoteza maisha yao nchini Iraq baada ya miji kadhaa ya nchi hiyo kushuhudia wimbi jipya la mashmbulio ya kigaidi. Vyombo vya usalama vya Iraq vinaripoti kuwa, miji ya Baghdad, Nainawa na al-Anbar hapo jana ilishuhudia mashambulio makubwa ya kigaidi yaliyopelekea kwa uchache watu 21 kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa. Taarifa zaidi zinasema kuwa, shambulio la kigaidi lililovilenga vikosi vya usalama katika kitongoji cha A'dhamiya limepelekea watu 16 kuuawa huku tisa kati yao wakiwa ni maafisa wa usalama. Aidha mlipuko wa bomu katika mji wa Mosul mkoani Nainawa umesababisha polisi wanne kuuawa na wengine wanane kujeruhiwa. Hayo yanajiri katika hali ambayo licha ya kupita miezi kadhaa tokea ulipofanyika uchaguzi wa bunge nchini Iraq, lakini hadi sasa nchi hiyo imeshindwa kuunda serikali mpya kutokana na hitilafu zinazotawala katika anga ya kisiasa ya nchi hiyo


Ethiopia yatiliana saini makubaliano ya amani na wapiganaji wa Ogaden


Serikali ya Ethiopia imetiliana saini makubaliano ya amani na wapiganaji wa jimbo la Ogaden wa Muungano wa Kupigania Ukombozi wa Magharibi mwa Somalia (UWSLF). Kwa mujibu wa makubaliano hayo, pande husika zimekubaliana kusitisha mapigano na kuwaachilia huru wafungwa wa pande mbili. Makubaliano hayo ya kusitisha uhasama yameelezwa kuwa yana nafasi muhimu katika mchakato wa amani nchini Ethiopia. Awali serikali ya Addis Ababa na kundi hilo la wapiganaji la United Western Somali Liberation Front (UWSLF) zilitiliana saini makubaliano ya kusitisha mapigano Aprili mwaka huu huko nchini Djibouti, makubaliano ambayo yaliandaa uwanja wa makubaliano haya ya mwisho. Hata hivyo kundi jingine la Harakati ya Ukombozi wa Ogaden ONLF linalopigania kujitenga eneo la Ogaden lenyewe limeyapinga makubaliano hayo na kusisitiza kuendeleza vita vyake dhidi ya serikali ya Ethiopia.

Thursday, July 29, 2010

Kapumzike kwa amani mpiganaji mwenzetu
Mume wa Marehemu Primitiva Pancras ambaye alikuwa mwandishi wa habari wa kampuni ya New Habari Cooparation 2006 Bw. Joachim Mushi akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya mke wake yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam,
Marehemu Primitiva alifariki juzi mkatika Hospitali ya Lugalo baada ya kuugua ghafla na kupoteza uhai wake,Marehemu atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuandika habari na makala zenye mguso kwa jamii hivyo kujipatia heshima kubwa kwa wasomaji wake ingawa alikuwa bado mchanga kwa kiasi fulani katika fani hii ya uandishi.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Primitiva Pancars AMEN.
Waombolezaji wakibeba Jeneza lililowekwa mwili wa Marehemu Primitiva Pancras tayari kwa mazishi katika makaburi ya Kionodoni leo.
Bw. Joachim Mushi ambaye ni Mhariri wa makala wa Gazeti la Jambo Leo akiuaga mwili wa marehemu mke wake Primitiva Pancras kwa majonzi makubwa wakati wa ibada ya kuaga mwili huo iliyofanyika kwenye kanisa katoliki la Hananasifu Kinondoni jijini Dar es salaam.
Hawa ni wakurugezni wa Gazeti la Jambo leo kulia ni Juma Pinto na kushoto ni Benny Kisaka wakishiriki katika ibada ya mazishi ya Mwandishi Primitiva Pancras, Marehemu Primitiva alikuwa ni mke wa Mwandishi wa habari na Mhariri wa makala wa Gazeti la Jambo leo Joachim Mushi.
Mpiganaji John Badi kutoka gazeti la This Day naye ameshiriki katika kuaga mwili wa marehemu Primitiva ni kweli alikuwa mtu wa watu.
Mpiga picha wa New Habari Cooparation 2006 Anthony Siame pamoja na muombolezaji mwingine wakimsaidia mmoja wa waombolezaji aliyeshindwa kujizuia mara baada ya kuona mwili wa marehemu Primitiva Pancras na kupoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo kwenye kanisa katoliki la Hananasifu Kinondoni leo.
Mdau Jerry Muro mbele kulia na mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima Absalom Kibanda nyuma pamoja na waombolezaji wengine wakiwa aktika ibada hiyo ya mazishi leo.
Mwanahabari Robert Komba ambaye ni mfanyakazi wa New Habari Cooparation 2006 kama mhariri wa Mtanzania Jumapili akiwapa pole wafanyakazi wenzie kushoto ni Mwandishi Siddy Mgumia na Mwanaharusi Pongwa ambaye pia ni mfanayakazi wa kampuni hiyo katika kitengo cha matangazo baada ya kuondokewa na kipenzi chao, mfanyakazi mwenzao Primitiva Pancras.
Ulikuwa ni wakati wa majonzi kwa ndugu na jamaa wa marehemu Primitiva Pancras wakati wa ibada ya kuaga mwili leo.
Waombolezaji na waandishi mbalimbali wakishiriki katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu Primitiva Pancras kwenye kanisa Katoliki la Hananasifu Kinondoni

Rais Karume Azindua Majenereta 32 Ya Umeme Wa Akiba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani AbeidKarume,akiweka mkono wake kujaribu upepo wa feni wa Jenereta baada ya kuiwasha
ikiwa ni hatua ya Uzinduzi wa majenereta 32 ya Umeme wa Akiba,huko Kituo Kikuu cha Umeme Mtoni,majenereta hayo yamewekwa na Kampuni ya Mantrac ya Nchini Misri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid
Karume,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa majenereta 32 ya umeme wa akiba yaliyowekwa na Kampuni ya Mantrac kutoka Nchini Misri,huko Kituo kikuu cha Umeme.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Amani Abeid
 Karume,akisisitiza jambo wakati alipotembelea Majenereta 32 ya Akiba,mara bada ya kuyazindua Huko Mtoni kituo Kikuu cha Umeme,(kulia) Mtaalamu wa Kampuni yaMantrac kutoka Nchini Misri Youseif Aly Youseif,Kampuni ya Mantrac ndioiliyoshuhulikia uwekaji wa Majenereta hayo,(kushoto) Waziri wa Maji,Ujenzi,Nishati na Ardhi,Mansour Yussuf Himidi
Haya ni Baadhi ya Majenereta 32 ya akiba ambayo yatasaidia wakati Umeme kutoka kidato utakuwa na matatizo,na kukosekanwa kwa muda,yakiwa kituo kikuu cha umeme Mtoni Mkoa wa Mjini Mahgaribi Unguja.Picha na Ramadhan Othman Ikulu/Zanzibar.


Dk Asha Rose Migiro Amtembela Rais Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar Es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rozi Migiro leo asubuhi.
Rais Jakaya Kikwete Akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rozi Migiro mara tu Baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es salaam na Kufanya naye Mazungumzo Leo asubuhi.Picha na Ikulu



Rais Jakaya Kikwete Amteua Balozi Francis Malambugi Kuwa Balozi Wetu Mpya Nchini Brazil
Balozi Francis Malambugi
--
Na Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amemteua Balozi Francis Malambugi kuwa Balozi wa Tanzania Brasilia nchini Brazil .
Uteuzi wa Balozi Malambugi umefuatia kutokana na aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Balozi Daktari Joram Mkama Biswaro kuteuliwa hivi karibuni kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika.
Balozi Malambugi ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria na Mwanadiplomasia alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 1/1/1978 kama Wakili wa Serikali na amewahi kufanyakazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Angola, Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Geneva, Ujerumani,Ethiopia na Ubelgiji.

Ajali ya boti Congo 'yaua 140'

Congo
Boti moja iliyokuwa imebeba abiria na bidhaa imepinduka kwenye mto katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kusababisha vifo vya takriban watu 140.
Ajali hiyo imetokea katika mto wa Kasai- vijito vya mto Congo- katika jimbo la Bandundu liliopo magharibi mwa nchi hiyo.Polisi wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa boti hiyo ilikuwa imejaa kupita kiasi.Baada ya miongo kadhaa ya migogoro, Kongo ina barabara chache au reli, inayosababisha wengi kusafiri kwenye boti hizo zilizojaa pumoni.Mwezi Novemba iliyopita takriban watu 73 walifariki dunia baada ya boti kuzama kwenye ziwa, pia katika jimbo la Bandundu.Ajali iliyotokea hivi karibuni ilitokea siku ya Jumatano.Boti hiyo ilikuwa ikibeba abiria na bidhaa kutoka Mushie, takriban kilomita 30 kutoka Bandundu, mji mkuu katika jimbo hilo.Ofisa polisi wa jimbo hilo Jolly Limengo ameliambia shirika la habari la Reuters, " Boti hiyo ilijaa pumoni na haikuweza kuhimili kupita kwenye dhoruba hiyo."

Mafuriko yasababisha vifo vya watu 40 mashariki mwa Afghanistan



Watu wasiopungua 40 wamefariki dunia huko mashariki mwa Afghanistan na mamia ya wengine wamebaki bila ya makaazi kutokana na mvua kali zilizosababisha mafuriko katika eneo hilo. Ripoti kutoka Afghanistan zinaeleza kuwa watu 15 pia wamejeruhiwa kutokana na mafuriko hayo. Kwa mujibu wa ripoti hizo watu hao 40 wakiwemo wanawake na watoto wamefariki dunia katika majimbo ya Kapisa na Laghman. Aidha mamia ya ekari za ardhi na nyumba zimesombwa au kuharibiwa na janga hilo la kimaumbile. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Udhibiti wa Majanga nchini Afghanistan, mnamo mwezi Mei, watu wasiopungua 66 walifariki dunia kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali zilizonyesha kwa siku kadhaa katika maeneo ya kaskazini na magharibi mwa nchi hiyo


12 wafariki dunia kwenye machafuko yanayoendelea mjini Mogadishu


Viongozi wa Serikali ya Mpito ya Somalia wamesema leo kuwa, watu wasiopungua 12 wameuawa na wengine 43 kujeruhiwa baada ya kutokea mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na waasi wa kundi la Hizbu Islam. Ali Mussa Sheikh afisa anayeshughulikia utoaji huduma za kwanza mjini Mogadishu amesema kuwa, mapigano hayo yameanza baada ya kundi la Hizbu Islam kushambulia kambi ya vikosi vya serikali karibu na Ikulu ya Rais wa Somalia. Ali Mussa Sheikh amesema kuwa, kikosi chake kimefanikiwa kuwaokoa majeruhi 43 na kuwapeleka hospitali. Makundi ya al Shabaab na Hizbu Islam yanapambana na majeshi ya serikali yanayosaidiwa na vikosi vya Umoja wa Afrika vya kulinda amani nchini humo, kwa shabaha ya kuiangusha serikali ya mpito ya Somalia inayoongozwa na Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmad.

Tuesday, July 27, 2010


JK Akutana Na Gaddafi Kampala
President Jakaya Mrisho Kikwete meets Libyan Leader Col.Muammar Gaddafi at Kampala Munyonyo international Conference centre during the on going 15th African union summit yesterday evening.President Jakaya Mrisho Kikwete(centre) the host President Yoweri Kaguta Museveni(right) together with Ethiopian Prime Minister Meles Zenawi(left) arrive for a closed session of the 15th African Union Summit, at Speke’s Resort Conference Centre in Munyonyo Kampala yesterday afternoon.
(photos by Freddy Maro)
Wyclef Jean Once Again Considers Running For President Of Haiti
Wyclef Jean is reconsidering running for president of his devastated homeland Haiti, according to his charitable foundation.

The former Fugees star has been instrumental in ensuring the Haitians left homeless by the massive earthquake in January have aid, and has built temporary shelters through his Yele Haiti organization.

Jean's dedication and service prompted many to call for him to step into politics, but he initially shrugged off the idea, saying, "If I take a job being a president, I can't do as much as I'm doing for my country."

However, according to 
CNN, the star has filled out the relevant paperwork in case he wants to put himself forward as a presidential candidate in the 2010 elections, pondering during a telephone interview, "I can't sing forever."

But a statement from his foundation adds that Jean is yet to come to a final decision: "Wyclef's commitment to his homeland and its youth is boundless, and he will remain its greatest supporter regardless of whether he is part of the government moving forward. At this time, 
Wyclef Jean has not announced his intent to run for Haitian president. If and when a decision is made, media will be alerted immediately."


*********************
DMX Is Going To Jail Again






Rapper DMX is heading back to jail just weeks after serving a four-month stint behind bars for a probation violation.
The gravel-voiced hip-hop star is planning to surrender to authorities and begin serving time in Los Angeles in connection to a reckless driving conviction eight years ago.
TMZ.com reports DMX was placed on probation after he pleaded no contest to the crime, which he has since violated and has been ordered to serve 90 days behind bars.
The rapper's manager insists her client, real name Earl Simmons, is "focused" on taking care of all of his past legal issues so he can move on with his life.
It's a dark time for DMX - the recently separated from his wife, according to reports.
Tashera Simmons, who wed the rapper in 1999, has stood by her husband throughout his legal troubles, but has decided enough is enough, according to Allhiphop.com.
Tashera is said to have confirmed the separation to the website and announced plans for a new reality TV series, which will show her rebuilding her life with the couple's four children following the split.
DMX

MARADONA ON BRINK OF LEARNING FATE



Diego Maradona's future as Argentina coach could become clear on Tuesday night when the federation president Julio Grondona discusses the details of Monday's meeting with his board.
Maradona said he would no longer coach Argentina after they were eliminated from the World Cup by Germany at the quarter-final stage, but on Monday morning he revealed he is keen to sign a new contract - so long as he is allowed to retain his entire backroom staff.
The 49-year-old met with Grondona in Ezeiza - a city close to Buenos Aires - on Monday, and the Argentinian Football Association (AFA) president will discuss the matter with board members on Tuesday night.
AFA spokesman Ernesto Cherquis Bialo told Radio La Red: "Maradona told the AFA president his thoughts about the present and future and what he was expecting regarding his staff. The president's idea was the opposite and they discussed about that.
"After both parties expressed their own points of view, Grondona told Maradona that he was going to communicate his requirements to the members' executive committee in tomorrow's meeting and, according to the decision they make, then they were going to meet again.
"The meeting went through different moments. Some of them were kind, some others tense, but talking about football always.
"Only Maradona and Grondona attended the meeting. Gossip and speculation by the media are just theories and hypothesis and I cannot say anything about that.
"The executive committee will be given a spoken review of the meeting by Grondona and, according to what he reports, the committee will make a decision or they could even delay it."
Reports suggest Grondona wants the 1986 World Cup winner to pen a new four-year deal, but one of Maradona's assistants, former Argentina defender Oscar Ruggeri, has been criticised by the AFA chief in the wake of the team's World Cup exit.
Argentina's next game is a friendly against Ireland on August 11 in Dublin, and the squad is due to be announced on Tuesday.
********************************

MILNER IN 'AMICABLE' VILLA TALKS


James Milner has been included in Aston Villa's squad for the Guadiana Cup in Portugal this weekend after holding "amicable" talks with club manager Martin O'Neill.
The 24-year-old returned to pre-season training today after being given a month's holiday following England's early exit from the World Cup.
Milner has been the subject of one £20 million bid already from Manchester City which was rejected by the midlands club.
He was reported to be upset last week after O'Neill had said the former Newcastle player had "intimated" he wanted to leave Villa.
But O'Neill is including Milner in his pre-season plans for the cup clashes with Feyenoord and Benfica on Saturday and Sunday respectively.
He and club chief executive Paul Faulkner met Milner and his representative, PFA executive Matthew Buck, after training at Bodymoor Heath today.

Villa issued a statement which reads: "James Milner trained with the rest of the Villa squad today at Bodymoor Heath.
"He and the manager, along with chief executive Paul Faulkner and the player's representative, Matthew Buck, had an amicable conversation.
"While James will not play in tomorrow's game at Walsall, he will fly with the squad to Portugal on Wednesday ahead of the Guadiana Cup in which Villa will compete with Benfica and Feyenoord this weekend."
O'Neill is waiting to discover whether City will lodge an improved bid for Milner who is valued at around £30 million.
But Harry Redknapp admitted Milner was out of Tottenham's price range as well as insisting he has made no approach for Villa winger Ashley Young.
Milner will be happy not to have to tread the same path as Gareth Barry in avoiding having to play against Walsall tomorrow evening.
Barry was the subject of much verbal abuse from Villa fans after he had made clear his desire to move to Liverpool in the corresponding friendly two summers ago.
He eventually stayed at Villa for another 12 months before moving.
Iran kuisaidia Kenya kujenga nyumba za kisasa kwa bei nafuu
Sample Image
Shirika moja la Iran limeafiki kufadhili ujenzi wa nyumba takribani 3000 nchini Kenya.Kwa mujibu wa mkataba wa maelewano uliotiwa saini kati ya Shirika la Mahun la Iran na Shirika la Taifa la Nyumba la Kenya-NHC- shirika hilo la Iran litatoa takribani shilingi bilioni sita kujenga nyumba hizo kwa teknolojia ya kisasa na ambazo watauziwa wananchi wa Kenya kwa bei nafuu. Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Nairobi jana katika kikao kilichohudhuriwa na balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya Dr Seyyed Ali Sharifi. Akizungmza katika kikao hicho Balozi Sharifi amesema kwa mtazamo wa Iran Kenya si lango la Afrika Mashariki tu bali ni lango la bara zima la Afrika


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akaribisha mazungmzo ya nyuklia ya Iran
Sample ImageKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha wazo la kuanza tena mazungmzo ya nyuklia kati ya Iran na Kundi la Vienna.
Msemaji wa Katibu Mkuu Martin Nesirky amewaambia waandishi habari mjini New York kuwa Ban daima amekuwa akiunga mkono kuanza upya mazungmzo. Kundi la Vienna linajumuisha Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, Russia, Ufaransa na Marekani. Wakati huo huo Balozi wa Iran katika IAEA mjini Vienna Ali Asghar Sultaniyeh, jana alimkabidhi mkuu wa wakala huo, Yukia Amano, barua rasmi ya Iran ambapo Tehran imetangaza kuwa tayari kufanya mazungumzo na Kundi la Vienna kuhusu ubadilishanaji mafuta ya nyuklia kwa ajili ya kinu cha nyuklia cha Tehran.

Monday, July 26, 2010

Chavez: Iwapo Venezuela itashambuliwa, hatutaipatia mafuta Marekani


Rais Hugo Chavez wa Venezuela ametishia kwamba, iwapo mivutano itaongezeka kati ya serikali ya Venezuela na Colombia na kuchukuliwa hatua za kijeshi dhidi ya Caracas, serikali ya Venezuela itachukua uamuzi wa kukatisha kusafirisha mafuta yake nchini Marekani. Uhusiano wa Venezuela na Colombia uliingia dosari wiki iliyopita na kupelekea kukatika uhusiano wa kidiplomasia wa pande hizo mbili, baada ya Rais wa Colombia kudai kwamba Venezuela inawahifadhi mamia ya waasi wa Colombia, suala ambalo limekadhibishwa vikali na serikali ya Venezuela. Rais Chavez ameamua kufuta safari yake aliyoipanga kuelekea Cuba kutokana na kuongezeka mivutano kati ya nchi hizo mbili. Rais Chavez amesema kuwa, nchi yake iko tayari kuzima jaribio lolote la kijeshi litakalofanywa na Colombia, nchi ambayo inahesabiwa kuwa ni kibaraka wa Marekani katika eneo la Amerika ya Latini.

JK IN KAMPALA FOR THE 15TH AFRICAN UNION SUMMIT


President Jakaya Mrisho Kikwete inspects guard of honor mounted by the Uganda People’s Defense Forces(UPDF) shortly after he arrived in the Ugandan Capital Kampala for the 15th African Union Summit yestarday afternoon.

President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Tanzanian Foreign Affairs Minister, Bernard Membe during the ongoing 15th African Union Summit at Munyonyo Speke Resort in Kampala.

President Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete receive bouquet of flowers upon arrival in Kampala for the 15th African Union Summit yestarday afternoon.
(photo by Freddy Maro)


FIESTA YAWADATISHA WAZANZIBARI NDANI YA NGOME KONGWE!!


Msanii kutoka Arusha anayejulikana kwa jina la Angel ametikisa Ngome Kongwe kwa jinsi alivyonyonga kiuno kama pia, kitu kilichowafanya mashabiki kumshangilia kwa nguvu wakati akiimba jukwaani katika tamasha la Fiesta lililofanyika usiku huu mjini Zanzibar na kushirikisha wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva.
Tamasha hilo linafanyika baada ya lile la Tanga lililofanyika jumamosi kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani humo na linadhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers (SBL) ya jijini Dar es Salaam.

Amini naye akafanya mambo makubwa katika tamasha hilo kama unavyomuona.
Mwasiti naye hakubaki nyuma, alikamua vilivyo na kuwapambanisha mashabiki ambao aliwaita vidume (hawapo pichani), yote ikiwa ni burudani tu.

Msanii huyu pia alikuwepo na akavuta hisia za mashabiki kwa staili yake.

Mr. Wise akitoa burudani na mrembo ambaye alivuta hisia za mashabiki wengi usiku huu na kushangiliwa kwa nguvu.

Mustafa wa G5 Click akiwa kazini Ngome Kongwe.

Barnaba na Nina wakitafuta muafaka wa SMS!

Binamu Mwana FA akiwarusha mashabiki wake.

Mashabiki tofauti wakiwa ndani ya Ngome Kongwe wakishuhudia vimbwanga vya wasanii.

Hapa Mwandishi Siddy akiwa na Nina na Barnaba.

Mdau Siddy Mgumia wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wasanii mbalimbali wa kike waliotumbuiza kwa nyakati tofauti katika tamasha la Fiesta Jipanguse mjini Zanzibar usiku huu.

Mkurugenzi wa Masoko SBL katikati akiwa katika picha ya pamoja na Teddy Mapunda wa pili kutoka kushoto, kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja Bidhaa SBL, Mr. Mapunda anayefuata na kushoto ni Godfrey Kusaga kutoka Prime Time.

Mdau Siddy Mgumia kushoto na Meneja mkuu Mawasiliano, Uhusiano na Jamii Teddy Mapunda wakiwa katika picha ya pamoja na Chui wa Serengeti katika tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 'Rrrrah'.

Meneja Mkuu Mawasiliano, Uhusiano na Jamii Teddy Mapunda kulia, Nandi Mwiyombela Meneja Bidhaa wa Serengeti pamoja na viongozi wengine wa kampuni ya SBL wakiwa katika Fiesta inayofanyika usiku huu Ngome Kongwe Zanzibar.
habari na full shangwe.