SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, November 10, 2010

Wafanyakazi wa Nigeria huenda wakaanza mgomo wao wa kudai mishahara hii leo

Wafanyakazi nchini Nigeria wanakusudia kuanza mgomo wao wa nchi nzima hii leo licha ya mazungumzo ya hapo jana kati ya viongozi wa jumuiya za wafanyakazi na Rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan. Rais wa Nigeria jana alikatisha ziara yake mjini Lagos ili kufanya mazungumzo na viongozi wa jumuiya mbili kuu za wafanyakazi nchini humo. Hata hivyo mwishoni mwa mazungumzo hayo yaliyochukua muda wa masaa matatu Promise Adewusi anayekaimu uongozi wa Congress ya wafanyakazi wa Nigeria NLC alisema licha ya wito wa kusitishwa uliotolewa na Rais Jonathan, mgomo huo utafanyika kama ilivyopangwa na kwamba ni kikao cha pamoja tu cha mabaraza ya utendaji ya jumuiya hizo mbili za wafanyakazi ndicho kinachoweza kutoa uamuzi wa kuusimamisha. Kikao cha mabaraza hayo kinatazamiwa kufanyika baadaye leo ili kutoa uamuzi juu ya suala hilo. Katika madai yake ya awali ya nyongeza za mishahara Congress ya wafanyakazi wa Nigeria iliitaka serikali iongeze kima cha chini cha mshahara kutoka naira 7,500 hadi 52,000 ambazo ni sawa na dola 346 za Kimarekani, lakini baadayae ikakubali kupunguza kima hicho hadi naira 18,000. Wafanyakazi wa kima cha chini hawajaongezewa mishahara kwa zaidi ya muongo mzima sasa nchini Nigeria

0 comments:

Post a Comment