Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba akihakiki fomu
alizorudisha Rais Jakaya Kikwete za kuwania urais kwa tiketi ya CCM
mjini Dodoma leo asubuhi.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwapungia mamia ya wanachama wa CCM waliojitokeza kushuhudia
akirudisha fomu za kuwania urais kwa tiketi ya CCM leo asubuhi katika
makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi.

Rais jakaya Mrisho kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete
wakiwasalimia mamia ya wanachama wa CCM waliojitokeza kumsindikiza
akirudisha fomu za kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na baadhi ya Wanachama wa CCM muda mfupi baada ya kurudisha
fomu za ugombea Rais kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi(picha
na Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment