SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, July 13, 2010

Al-shabab yakiri kuhusika na milipuko ya Kampala iliyoua watu 74
Sample Image
Msemaji wa kundi lenye misimamo mikali la Al Shabab la Somalia amekiri kuwa kundi hilo limehusika na mashambulizi mawili ya mabomu yaliyolenga watu waliokuwa wakitazama fainali ya Kombe la Dunia jana usiku mjini Kapala, Uganda. Ali Muhammad Rage amesema kundi la Al Shabab limehusika katika mashambulizi hayo na kwamba iwapom askari wa Uganda wataendelea kuua Wasomali basi kundi hilo litaendelea mashambulizi yake. Amedai kwamba mashambulizi hayo yamefanywa kulipiza kisasi cha mauaji ya Wasomalia wanaouawa na askari wa Uganda. Wakati huo huo kamanda wa ngazi za juu wa kundi la Al-shabab amesema kuwa amefurahishwa mno na milipuko miwili ya mabomu iliyotokea usiku wa jana mjini Kampala Uganda na kusababisha vifo vya watu 74. Sheik Yusuf Sheik Issa amesema kuwa Uganda ni adui wa kundi hilo na chochote kinachoiliza nchi hiyo basi ni furaha kwa Al-shabab. Makumi ya watu pia walijeruhiwa kwenye milipuko ya jana iliyotokea wakati watu walipokuwa wakitazama mechi ya fainali ya Kombe la Dunia kati ya Uhispania na Uholanzi. Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametoa mkono wa pole kwa wahanga wa mashambulio hayo na kuahidi kuwa serikali itafanya juu chini kuwatia nguvuni waliohusika.
Iwapo itabainika kuwa Al Shabab imehusika basi itakuwa mara ya kwanza kwa kundi hilo kufanya mashambulizi nje ya mipaka ya Somalia.

0 comments:

Post a Comment