SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.
Showing posts with label Waziri wa Mawasiliano. Show all posts
Showing posts with label Waziri wa Mawasiliano. Show all posts

Wednesday, April 23, 2014

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa Afungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala akisisitiza umuhimu wa mkutano wa wadau wa TEHAMA katika nchi za Bonde la Ufa na msatakabali wa vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia kwenda dijiti
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau  wa Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Mngondo (kulia) akiwa miongoni mwa washiriki wa mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la Ufa leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (katikati) akisalimiana na baadhi ya washiriki mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.Picha zote na Eleuteri Mangi
---

Na Eleuteri Mangi

Serikali imejenga mazingira mazuri kwa wawekezaji ili kuvutia makampuni mbalimbali kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano nchini. 


Kauli hiyo imemtolewa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.


“Nawasihi wajasiriamali katika mambo ya TEHAMA ndani ya nchi washirikiane na wenzao wa nje ya nchi ili waweze kujijengea uwezo wa kukuza uchumi wa nchi yetu” alisema Prof. Mbarawa.


Prof. Mbarawa aliwasihi washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania inawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika TEHAMA ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma ya mawasiliano katika maeneo yote nchini hadi vijijini.


Aidha, Prof. Mbarawa alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya TEHAMA ni pamoja na ukosefu wa nishati ya umeme vijijini, kumudu gharama za uendeshaji, ukosefu wa vifaa vya sekta hiyo na usalama wa taarifa mbalimbali katika mitandao.


Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa Bunge kutoka Burundi, Tharcisse Nkezabahizi alisema kuwa TEHAMA ni moja ya Nyanja muhimu inayotumiwa katika nchi yake ikiwemo elimu na huduma za afya ambapo ni muhimu kwa nchi za bonde la ufa kutumia teknolojia hiyo ili kukuza uchumi wan chi husika.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala alisema kuwa mkutano huo umekuja wakati mwafaka ambapo nchi nyingi zinatumia fursa iliyopo ili vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia kwenda dijiti.


Tanzania mpaka sasa imekuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika kutekeleza hatua ya kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda dijiti mbapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu takribani mikoa yote itakuwa imezima mitambo ya analojia kwenda dijiti.


Nchi zinazoshiriki katika mkutano huo ni Burundi, Rwanda, Somaliland, Zambia, Sudani Kusini ikiwemo Tanzania ambayo imekuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa mara ya pili mfululizo pamoja na wadau wengine katika sekta hiyo.

Tuesday, October 22, 2013

WAZIRI WA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA AZINDUA PRO.MBARAWA AZINDUA MPANGO WA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI KUUNGANISHWA NA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO


Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia  Profesa Makame Mbarawa, akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ukianzia Shule ya Kambangwa Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni  Meneja wa Samsung Tanzania  Kishor Kumar, wapili ni Mkuu wa kitengo cha mfuko wa huduma za jamii cha Vodacom,  Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,kutoka  kushoto ni  Mkuu wa shule  hiyo Bi.Theresia Ng’wigulu.

Sunday, April 21, 2013

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza,juu ya sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini

  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akimkaribisha ofisini kwake jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza ambapo baadae viongozi hao walifanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Masuala ya Sheria wa Vodacom Tanzania Bw.Walarick Nittu wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania(katikati)akiwa na ujumbe wake walipomtembelea Waziri Prof:Mbarawa na kuwa na mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Mitandao wa Vodacom Tanzania Bw. Alec Mulugo wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania(kulia)akiwa na ujumbe wake walipomtembelea Waziri  wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof: Mbarawa na kuwa na mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.