Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( Wa nne
kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa shughuli za
utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta mara baada ya kufungua warsha
hiyo. Picha na Asteria Muhozya.
Mmoja
wa wadau wa shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi akitoa maoni yake
kuhusu namna ya kuboresha rasimu ya Sera ya Petroli. Wanaofuatia ni
baadhi ya wadau kutoka Kampuni mbalimbali zinazofanya shughuli hizo nchini.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (katikati) akifuatilia kwa karibu wadau wakitoa maoni wakati wa warsha ya wadau wanaoshughulika na shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta ili kupata maoni yao yatakayosaidia kuboresha Rasimu ya Sera ya Petroli.
Wa
Kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Umeme
Mhandisi Innocent Luoga, wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi Nishati, anayeshughulikia Petroli Mhandisi Stanley Marisa na wa kwanza kulia ni Mjiolojia Mwandamizi Wizara ya Nishati na Madini, Adam Zuberi.
Washiriki katika warsha ya wadau wanaoshughulika na shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi na mafuta ili kupata maoni yao yatakayosaidia kuboresha Rasimu ya Sera ya Petroli
NA SUFIANI MAFOTO