Thomas Muller alifunga mabao matatu na kuisaidia Ujerumani kuishinda Ureno mabao manne kwa nunge.
Mlinzi wa Ureno, Pepe alionyeshwa kadi nyekundu na kuondolewa katika mchuano huo.
Ujerumani, mabingwa mara tatu wa kombe la dunia, walionyesha mchezo wa kiwango cha juu.
Ujerumani
ilichukua uongozi pale ambapo Thomas Muller alipopiga mkwaju wa
penalti, baada ya Joao Pereira kuchezea vibaya Mario Goetze.
Mart Hummels alifunga bao la pili kupitia kichwa.
Pepe alionyeshwa kadi nyekundu muda mfupi baadaye kwa kosa la kumgonga Muller kwa kichwa.
Muller alifunga bao la tatu, ambalo lilikua lake la pili katika mchuano huo, kwa mkwaju wa kutoka karibu na lango.
Katika
dakika ya 77, Thomas Muller aliongeza bao la nne la Ujerumani na
kufanya idadi ya mabao yake katika mchuano huo kuwa matatu.
Muller anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja, kwenye kombe hili la dunia, mwaka 2014.
Kufuatia ushindi huu, Ujerumani inaongoza kundi hili kwa alama tatu.
Chanzo BBC Swahili