SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, June 15, 2014

Picha;Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi abariki tamasha la 17 la ZIFF 2014 visiwani Zanzibar

DSC_0157
Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisalimiana na baadhi ya wageni alipowasili kwenye ufunguzi wa Tamasha la 17 la ZIFF Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF Mh. Mahmoud Thabit Kombo.Picha na Zainul Mzige
DSC_0159
Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisalimiana na Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto ambayo ilifungua tamasha hilo la 17 la ZIFF usiku wa kuamkia leo visiwani Zanzibar.
DSC_0158
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Wananchi Group ambao ni wadhamini wa ZIFF kupitia ZUKU, Bw. Mohammed Jeneby wakati wa tamasha hilo.
DSC_0164
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.
DSC_0174
DSC_0234
Pichani juu na chini ni kikundi cha burudani cha TANURI kutoka Egypt wakitoa burudani kwenye tamasha la 17 la ZIFF.
DSC_0300
DSC_0289
DSC_0386
Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando akimkaribisha Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto kwenye jukwaa.
DSC_0391
Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto akielekea jukwaani wakati wa ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF 2014.
DSC_0391
DSC_0395
Picha juu na chini Mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto, akizungumzia changamoto mbalimbali na mafanikio aliyoyapata baada ya kushiriki kwenye filamu hiyo.
DSC_0409
DSC_0414
Mmoja wa wageni waalikwa akimpongeza mgeni maalum mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry Pheto kwa kazi nzuri aliyofanya kupitia filamu yake.
DSC_0217
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais Balozi Sefu Iddi jukwaani kuzindua rasmi tamasha hilo.
DSC_0213
Mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisoma hotuba wakati akizindua rasmi wa Tamasha la 17 la filamu la nchi za Majahazi (ZIFF) linaloendelea kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.
DSC_0344
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) akimtambulisha mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed (kulia) kwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi.
DSC_0348
Mwakilishi wa Com-Net Zanzibar Bw. Mohammed akikambidhi zawadi ya kifurushi cha Internet ya mwaka mzima mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi .
DSC_0351
Mgeni rasmi Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akimshukuru mwakilishi wa Com-net mmoja wa wadhamini wa tamasha hilo kwa zawadi hiyo.
DSC_0332
Mkurugenzi Wananchi Group ambao ni wadhamini wa ZIFF kupitia ZUKU, Bw. Mohammed Jeneby akizungumzia udhamini wao wa miaka 10 kwenye tamasha hilo ambapo kwa sasa lina mwaka wa tatu.
DSC_0490
Meza kuu ikifuatilia filamu ya "Long Walk to Freedom" inayozungumzia maisha ya MANDELA wakati wa ukombozi wa mtu mweusi kutoka kwa makaburu.
DSC_0375
Mwigizaji Terry Pheto akifurahia jambo wakati wa kutazama filamu yake.
DSC_0342
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na mabalozi kwenye ufunguzi wa tamasha la 17 la ZIFF.
DSC_0370
Picha juu na chini wakazi wa Zanzibar na wageni mbalimbali kutoka nje ya Tanzania wakitazama filamu ya "Long Walk to Freedom kwenye ukumbi wa Ngome Kongwe linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF.
DSC_0317
DSC_0316
DSC_0431
Mwigizaji Terry Pheto akipozi na mmoja wa ushers waliokuwa wakikaribisha wageni kwenye tamasha hilo.
DSC_0574
Mdau Lucy (wa pili kushoto) katika pozi na picha yake kwenye viunga vya Ngome Kongwe wakitoa huduma ya vinywaji.