Dunia
ina hesabu masaa kabla ya kuanza kushuhudia faina za kombe la dunia
nchini Brazil huku kila timu ikijifua zaidi nchini humo huku usalama
ukiwa umepigiwa msitari na jeshi la Brazil. Ulinzi mkali wa jeshi unaousindikiza msafara wa timu hiyo popote uendapo uligeuka kero na kikwazo kwa wenyeji wa miji ya Brazili itakayoshuhudia mechi za fainali hizo zikichezwa.
Mjini Rio de
Janeiro hali imekua ngumu kwa wakazi wa mji huo hususan inapofika wakati
timu zinapokwenda katika viwanja vya kufanya mazoezi ya kujiandaa na
michezo ya kombe la dunia itakayowakabili kuanzia siku ya Al-khamisi ya
wiki hii.
Jana wakazi
wa jiji hilo walilazimika kusubiri kwa dakika 15 wakiwa barabarani kwa
ajili ya kupisha msafara wa timu ya taifa ya Uingereza ambayo imepangiwa
kufanya mazoezi kwenye kambi ya jeshi katika eneo la Urca.
Kimbembe cha
kusubiri kwa muda huyo wakiwa katika foleni kilisababishwa na
mshambuliaji wa klabu ya Everton Ross Barkley, ambae almanusura aachwe
hotolini baada ya kushindwa kwenda na muda wa kujiandaa kabla ya kuingia
kwenye basi kwa ajili ya kwenda mazoezini.
Tayari
wachezaji wenzake walikuwa wameshaingia kwenye basi na msafara ukataka
kuanza lakini ikabainika Ross Barkley hayupo garini, hivyo iliwalazimu
maafisa wa timu ya taifa ya Uingereza kuwaomba walinzi wa kambi yao
kufanya subra ambayo ilisababisha foleni kubwa.