Mjumbe wa Kamati ya Urasimishaji wa Kazi za wasanii wa Filamu na Muziki hapa nchini ambaye pia ni Afisa kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Wilhad Tairo akifafanua jambo kwa mfanyabiashara wa duka la Filamu wakati wa Operesheni ya kukagua Bidhaa zisizo kuwa na Stempu za TRA, Operesheni hiyo ya wiki mbili iliyoanza jana jijini Dar es Salaaminatekelezwa kwa uhirikiano wa TRA, Bodi ya Filamu, Basata na Cosota
Mfanyabiashara wa duka CDs za Filamu lililopo maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam akieleza jambo kwa maafisa wa Kikosi kazi kwa ajili yakukagua bidhaa ambazo azizingatii taratibu kabla ya kuingizwa sokoni leo jijini Dar es Salaam.
Muuzaji wa duka la CD za Filamu katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam akiwaonyesha Stempu za TRA katika CD zake wakaguzi kutoka TRA,Bodi ya Fila, Basata na Costa ambao walifika dukani kwake kwa ajili ya ukaguzi wa bidhaa ambazo zimeingizwa sokoni bila kufuata taratibu za kisheria iliwemo kuweka Stika za TRA kama sheria inavyotaka.Kamati ya urasimishaji wa kazi za wasanii wa Filamu na Muziki wameanza Operesheni ya wiki mbili katika jiji la Dar es Salaam ili kuleta ufanisi katika mapato ya Wasanii.
Afisa Kodi Msaidizi Bi. Theophilda Majara( Mwenye blauzi nyekundu) akikagua uhalisi wa Stempu za TRA katika CD za Filamu leo jijini Dar es Salaam wakati wa Operesheni ya kukagua na kukamata Filamu zitakazo kuwa hazijafuata utaratibu wa kisheria wa kuweka Stika na kusajili katika mamlaka husika.
Mfanyabiashara wa duka la CDza Filamu nchini akisoma kanuni za stempu za bidhaa za Filamu na Muziki zilizo china ya sheria ya ushuru wa bidhaa walipotembelewa na Kikosi kazi kinachofanya Operesheni ya kukagua bidhaa hizo ambazo zimeingia sokoni bila kuzingatia taratibu na matakwa ya sheria hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Kodi Msaidizi Bi. Theophilda Majara( Mwenye blauzi nyekundu) akikagua baadhi ya CD za Filamu wakati wa Operesheni ya kukagua Filamu ambazo hazijafuata taratibu za kisheria ikiwemo kulipia Stempu ya TRA kabla ya kuingia sokoni. Zoezi hilo linaendeshwa kwa ushirikiano wa TRA, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Bodi ya Filamu, Basata na Costota .
Baadhi ya wananchi wakifuatilia namna Operesheni ya kukagua Filamu zilizoingia sokoni bila kufuata utaratibu namna inavyotelekelezwa jana katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija