Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (PE. 1656) akila kiapo rasmi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian Matembele kwa mujibu wa sheria ya usajili wa wahandisi (Engineer's Registration Act (Cap 63), Kanuni na sheria ndogo zote zilizowekwa na zitakazowekwa ikiwemo mwendo wa utendaji kazi pamoja na maadili katika taaluma ya uhandisi.
Kiapo hicho kimeafanyika leo katika ukumbi wa "video comference" uliopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo tarehe 23-05-2014. Awali kiapo hicho kilikuwa kifanyike Dodoma pamoja na mawaziri na wabunge wengine ambao ni wahandisi lakini kutokana na majukumu yasiyozuilika Eng. Manyanya ameruhusiwa aape akiwa Sumbawanga.

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa kushoto akizungumza katika hafla hiyo. Alisema kuwa kwa upande wa wataalamu wa uchumi wanachangia sana katika kuongezeka au kuzorota kwa maendeleo ya nchi lakini hakuna utaratibu rasmi wa kusajiliwa na kuapishwa, Aliongeza kuwa pengine ingekua hivyo wataalamu hao wangekuwa makini zaidi katika kupanga mipango ya nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta kulia akitoa salam zake katika hafla hiyo. Katika salam hizo alitoa pongezi nyingi kwa niaba ya viongozi wote wa Mkoa wa Rukwa na wananchi kwa ujumla kwa Eng. Manyanya kwa kuwa mfano kwa kuapa kama ambavyo matakwa ya sheria ya usajili wa uhandisi inavyomtaka. Hiyo imekua ni chachu kwa wengine wote ambao hawajajisajiliwa na kuapa waone ni muhimu sasa kufanya hivyo. Kiapo hicho kinatoa funzo kwa watumishi wa kada zote kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo wa hali ya juu.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (katikati waliokaa) na Wakuu wa Idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa (nyuma waliosimama). Wengine kushoto waliokaa ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Rukwa Msomi Enock Kasian na Bi. Z. A. Mpangule Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Sumbawanga kulia.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na baadhi ya wahandisi waliosajiliwa na ambao hawajasajiliwa kutoka Mkoa wa Rukwa (nyuma waliosimama) muda mfupi baada ya kuapishwa.

Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa(Rukwareview.blogspot.com)
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa(Rukwareview.blogspot.com)