SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, May 11, 2014

AVEVA ACHUKUA FOMU KUWANIA URAIS KLABU YA SIMBA


Umati uliomsindikiza Aveva kuchukua fomu.
Aveva akikabidhiwa fomu yake ya kugombe Urais


Alipoingia alitoa kadi yake ya uanachama kujitambulisha kwa mtoa fomu, kisha kukabidhi ada na kupewa fomu yake kabla ya kuondoka kwa maandamano mazito.
Wakati wa maandamano wanachama walikuwa wakisukuma gari ya Aveva kuanzia Lumumba hadi makao makuu na mgombea huyo alikuwa akionyesha ishara ya vidole vitatu, akimaanisha sera yake ni pointi tatu- maana yake ushindi.
Na alipofika makao makuu wanachama ambao walikuwa hapo wakimsubiri nao walimlaki kwa shangwe, wakisema; “Huyu ndiye rais wetu,”.
Kwa ujumla mapokezi ya Aveva yanaweza kuwakatisha tamaa watu wengine kujitokeza kuwania nafasi hiyo, kwani Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Usajili ameonekana kuungwa mkono na watu wengi.
Ni mtu mmoja tu hadi sasa ambaye tayari amechukua fomu ya Urais mbali na Aveva, ambaye ni Andrew Tupa, lakini habari zinasema mwanachama mwingine maarufu wa klabu hiyo,  Michael Richard Wambura naye atachukua fomu ya nafasi hiyo kesho.
Kihistoria Aveva ni Simba damu ambaye amekuwa akiisaidia klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 20 sasa ni miongoni mwa waasisi wa kundi la Friends Of Simba (F.O.S.), ambalo limekuwa na msaada mkubwa wa kifedha katika klabu hiyo.

Hajawahi kuwa kiongozi wa kuchaguliwa, lakini amekwishaongoza kwa mafanikio Kamati kadhaa, ikiwemo ya Usajili mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambayo ilifanya kazi nzuri ya kuibua vipaji kama vya akina Boniface Pawasa, Ulimboka Mwakingwe, Emmanuel Gabriel, Juma Kaseja, Yahya Akilimali, Said Maulid ‘SMG’, Suleiman Matola na wengine wengi. Habari na picha kwa hisani ya Bin Zubeiry