Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akiongea na waandishi
wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa Mpesa
kwenye vituo vya mafuta vya Total nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa
Biashara wa Total Romee de Villeneuve. Uzinduzi huo umefanyika leo
jijini Dra es salaam.
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim akiwaonesha waandishi
wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kulipia mafuta kwa Mpesa kwenye
vituo vya mafuta vya Total muda mfupi baada ya kuzinduliwa rasmi kwa
huduma hiyo kwenye kituo cha Total cha Morocco jijini Dra es salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de Villeneuve. Huduma
hiyo itakuwa ikipatikana kwenye vituo vyote vya Total hapa nchini.
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim (wa pili kushoto)
akimsadia dereva Taxi Said Juma kulipia mafuta kwa njia ya M-pesa katika
kituo cha Mafuta cha Totola Morocco jijini Dar es salaam akiwa ndie
mteja wa kwanza kutumia huduma hiyo muda mfupi baada ya kuzinduliwa
kituoni hapo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Total Romee de
Villeneuve na kulia ni mhudumu wa kituo hicho Malaki Peter. Huduma hiyo
itakuwa ikipatikana kwenye vituo vyote vya Total nchini.
Wafanyakazi
wa Vodacom wa idara ya mauzo wakibandika stika kwenye kituo cha mafuta
cha Total Morocco jijini Dar es salaam zinazoonesha nambari ya biashara
ya kulipia huduma ya mafuta kwa njia ya Mpesa kituoni hapo. Huduma hiyo
imezinduliwa kituoni hapo na kwamba itapatikana kwenye vituo vyote vya
Total nchi nzima ikiwa ni mwendelezo wa Vodacom kuwawezesaha watanzania
kupata huduma kwa urahisi, uhakika na usalama kupitia huduma ya M-pesa.
Mfanyakazi
wa kituo cha mafuta cha Total Morocco jijini Dar es salaam akitoa
huduma ya mafuta kwa wateja. Total na Vodacom imezindua ubia wa
kibiashara unaowawezesha wateja kulipia huduma ya mafuta kwa M-pesa
kwenye vituo vyote vya Total nchi nzima. Huduma hiyo inalenga kutoa
unafuu na urahisi wa malipo kwa wateja.
Waendesha
vyombo vya moto barabarani wamerahisishiwa njia ya kununua na kulipia
mafuta kwa njia ya M-Pesa, kufuatia ushirikiano kati ya kampuni ya simu
za mkononi Vodacom M-Pesa na kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta
ya Total Tanzania.
Ushirikiano
huo umeanzia kwenye vituo vichache vya Total Tanzania na baadae
kusambaa maeneo mbalimbali nchini, lengo kuu ni kuhakikisha kila
mtanzania anaemiliki chombo cha moto anakuwa na uwezo wa kununua na
kulipia mafuta kwa njia iliyo salama na uhakika.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,
Salum Mwalim, amesema siku zote kampuni yake imekuwa msitari wa mbele
katika kurahisisha maisha ya Watanzania kupitia miundombinu ya
kiteknolojia iliyo nayo.
"Tumekuwa
tukibuni njia mbalimbali kila siku kwa lengo la kuwapa urahisi wateja
wetu na kuwaondolea adha ambazo wanaweza kuzipata wakiwa wanataka
kununua mafuta kutoka vituo vya Total Tanzania, sasa wateja wetu wote
kupita M-Pesa ambayo siku izi imechukua nafasi kubwa sana katika mfumo
wa maisha ya binadamu wana uwezo wa kununua na kulipia mafuta kutoka
vituo ivyo vya mafuta." Alisema Mwalim
Aidha,
Mwalim aliongeza kuwa kampuni ya Vodacom kupitia M-Pesa wataendelea
kuwaletea wateja mambo mengi ambayo hayajawahi kutokea nchini, lengo
likiwa ni kuhakikisha biashara zote nchini zimeunganishwa na M-Pesa ili
kwenda sambamba ambapo hadi sasa tayari biashara zaidi ya 320
zimeshaunganishwa na huduma hiyo.
"Tunatambua
watu wengi wanahitaji la kununua mafuta kwa ajili ya magari au piki
piki zao lakini kwa bahati mbaya wanaweza kufika kwenye kituo cha mafuta
wakiwa na fedha pungufu, sasa wasiwe na wasi wasi wowote endapo
watakuwa na fedha katika akaunti zao za M-Pesa wanaweza kutatua tatizo
hilo". Alisisitiza Mwalim.
Kwa
upande wake Meneja wa Maendeleo, Ubora na Mafunzo wa Kituo cha mafuta
cha Total Tanzania, Maria Lebby, Amesema kupitia njia hii wateja wa
Total watanufaika kutokana na namna kampuni hiyo ilivyo jidhatiti katika
kurahisisha njia za malipo.
"Tumekuwa
tukipokea wateja mbalimbali kwa nyakati tofauti zikiwemo za usiku
ambazo ni hatarishi kwa usalama wa fedha alizobeba mteja, hivyo basi
kuanzia sasa mteja wetu anaweza kutembea bila yakubeba fedha taslimu na
badala yake kuziweka kwenye akaunti yake ya M-Pesa na kujihakikishia
anapata huduma akiwa na amani juu ya usalama wa fedha zake."
Aidha
Meneja huyo aliendelea kubainisha manufaa watakayopata wateja kwa kusema
"huu ni wakati wakutumia teknolojia tulizonazo ili kurahisisha
upatikanaji wa huduma kwa watanzania, waliowengi wanapenda kufanya mambo
yao kwa uharaka hasa wanapokuwa na majukumu mengine yakufanya, kupitia
huduma hii tatizo hilo litakuwa limetatuliwa".
"Natoa
wito kwa makampuni mengine kukubali kupokea mapinduzi yanayoletwa na
teknolojia ili kuweza kwenda na wakati na kurahisisha mfumo mzima wa
upatikanaji wa huduma". Alihitimisha Lebby.