SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, April 12, 2014

Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) watinga Bungeni mjini Dodoma

injinia
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Habib  Mnyaa akitoa ufafanuzi  leo kuhusu  maoni  ya  taarifa ya Kamati Namba Moja ya Bunge la Maalum la Katiba.  
kilango
Mwenyekiti  wa Kamati Namba  Kumi na Moja  ya Bunge Maalum  la Katiba, Anna Kilango Malecela akiwasilisha leo  taarifa ya Kamati yake kuhusu Sura ya kwanza na sura ya sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
bingwa
Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) ikiwa katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya  timu  hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba leo.
mwenyekiti
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta akijadiliana jambo na mjumbe wa Bunge hilo, Vita Kawawa leo mjini Dodoma wakati wa  kikao.
frank william
Mfungaji bora wa wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) na Kapteni Msaidizi  Emmanule Amos akipeana mkono na Makamu wa pili  wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya  timu  hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba  leo.
naibu-waziri
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake  Juma Nkamia wakiwa wameshikilia Kombe la  ushindi la Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC)baada ya timu hiyo kutembelea Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo.
kocha
Mkurugenzi wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC), Mutani  Yangwe akisalimiana na  Makamu wa pili  wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya  timu  hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba  leo.
kipa
Kipabora  wa Timu ya Watoto wa Mitaani (TSC) na Kapteni Msaidizi  Emmanule Amos akipeana mkono na Makamu wa pili  wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi mjini Dodoma mara baada ya  timu  hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba leo .
kombe
Makamu wa pili  wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara  wakiwa  wameshikilia  Kombe la Dunia  la Ushindi  wa  Mashindano ya Watoto wa Mitaani  leo mjini Dodoma mara baada ya  timu  hiyo na viongozi wao kutembelea Bunge Maalum la Katiba .
(Picha  zote na Kamati ya Bunge Maalum la Katiba).