SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, April 10, 2014

Ripoti Za Kamati Za Bunge Maalum la Katiba Zakabidhiwa Rasmi Kwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Mjini Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati namba  kumi na mbili ya Bunge Maalum la Katiba, Paul  Kimiti( kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan (kushoto) ripoti ya Kamati yake kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati namba  kumi na moja ya Bunge Maalum la Katiba, namba mbili, Shamsi Vuai Nahodha( kulia)akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan(kushoto) ripoti ya Kamati yake kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati namba  kumi  ya Bunge Maalum la Katiba, Anna Abdallah (katikati)akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan(kulia) ripoti ya Kamati yake kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma jana .Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salmin Awadh Salimin.
Kaimu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba, John Joel akiwakarisha baadhi ya viongozi wa Kamati za Bunge hilo ili kuweza kukabidhi ripoti zao kwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan (kushoto)
Baadhi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakijadiliana jambo. Picha na Kamati ya Bunge Maalum la Katiba