SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, April 13, 2014

MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 30 YA KIFO CHA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE WILAYANI MONDULI

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishiriki misa maalum ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika nyumbani kwake Monduli. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenera Mkungara, na motto wa Marehemu sokoine Ndugu Joseph Sokoine.
Baadhi wa Waheshimiwa wabunge na Wabunge wakifuatilia misa kwa makini.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowasa, wakishiriki Misa maalum ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili kushiriki misa ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.
Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameketi na wajane wa hayati Edward Moringe Sokoine pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa katika misa ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.
Mhe. Rais akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim nae akiweka shada la maua.
Mhe. Lowasa nae akiweka shada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.
Mwakilishi wa Ujumbe wa wajumbe wa Bunge Maalum Mhe. Paul kimiti nae akiweka shada la Maua. Picha na Owen Mwandumbya.