SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, April 14, 2014

ABIRIA WA MIKOANI WAKWAMA DARAJA RUVU, BARABARA, DARAJA VYAJAA MAJI

 Wasafiri kutoka mikoani kuelekea jijini Dar es Salaam, waliokuwa wakisafiri jana wakiwa eneo la Ruvu Darajani wakitafakari jinsi ya kuvuka eneo hilo baada ya barabara kujaa maji na kushindwa kuvuka kwa mabasi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.
 Baadhi ya abiria waliamua kutembea na kuvuka kwa miguu baada ya kushushwa na mabasi waliokuwa wakisafiria katika eneo hilo, ambapo huvuka hadi upande wa pili na kupanda usafiri mwingine ambao unakuwa unageuzia eneo hilo pia.
Baadhi ya magari yaliyokwama kuvuka eneo hilo yakiwa katika msongamano huku kukiwa na usimamizi wa askari polisi.
CHANZO: NA SUFIANIMAFOTO