Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akiwa na Mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Cherie Blair wakati uzinduzi rasmi wa mradi wa Tigo Pesa kwa ajili ya kuboresha mfuko mpya wa Wezesha Wanawake kwa Maendeleo.
.Mwaka jana walizindua mpango wa Wezesha Wanawake kwa Maendeleo
.Wanawake wengi sasa wameweza kujiendeleza kibiashara na kuhudumia familia zao kwa ubora zaidi.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
JUMAMOSI
ya leo, Tanzania inaungana na nchi zingine duniani kuadhimisha siku ya
kimataifa ya wanawake ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika katika
kutambua mchango wa wanawake kuanzia ngazi ya kaya, taifa na kimataifa.
Siku
ya wanawake duniani ni siku ya kimataifa na dunia nzima huadhimisha
siku hii ya kipekee kwa kufurahia mafanikio yaliyopatikana kiuchumi,
kisiasa na kijamii kwa upande wakinamama.
Na
katika baadhi ya nchikama China, Urusi, Vietnam na Bulgaria siku hii ni
mapumziko ya kitaifa na hii yote ni katika juhudi za kutambua mchango wa
wakinamama katika kuleta mabadiliko katika jamii.
Ni
katika kuadhimisha siku hii muhimu wanawake wote duniani huja pamoja na
kutafakari jinsi ya kuendelea kumuelimisha mwanamke na kama usemi
maarufu usemao, ukimwelimisha mwanamke ni sawa na kuelimisha jamii
nzima.
Hapa
nyumbani kwa miaka ya hivi karibuni wanawake wamekuwa wajasirimali
wazuri na wenye msaada mkubwa katika familia (kaya) na taifa kwa ujumla.
Siku
ya Jumatatu mwezi Julai, mwaka jana, Tigo Tanzania kwa kushirikiana na
Taasisi ya Cherie Blair kwa ajili ya wanawake (CBFW), USAID na FINCA
walizindua mpango mkakati wa wanawake wajasiriamali.
Hiyo
yote ni kuonyesha ni kwa vipi kampuni hiyo yaTigo Tanzania
inavyothamini jamii kwa kuweza kurudisha sehemu ya mapato yake kwa
wananchi kupitia kitengo chake cha Huduma kwa Jamii (CR) ili kumwezesha
mwananchi wa kawaida na hasa mwanamke mwenye kipato cha chini.
Mpango
huo unajulikana kama Wezesha Wanawake kwa Maendeleo, umelenga kuwapa
uwezo wanawake zaidi ya 3,200 ambao ni mawakala wa Tigo pesa nchini, kwa
kuwapa elimu ya kutunza fedha na kupata masoko katika biashara zao.
Wakati
wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Tigo, Diego Gutierrez alisema lengo la
mpango huo ni kuwapatia fursa wanawake mawakala wa Tigopesa.
“Kwa
mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, wanawake wanamiliki karibu
asilimia 70 ya uchumi wa Afrika, kwa hiyo Tigo inajisikia fahari na
heshima kushirikiana na Taasisi ya Cherie Blair, USAID na FINCA katika
kutengeneza mazingira ambayo yatawahakikishia wanawake nafasi ya kupata
misaada ya kifedha, masoko, mafunzo na mawasiliano ya teknolojia,”
“kwa
ushirikiano wetu huu na wenzetu tutaweza kubuni miradi mingi kwa
wanawake wa Tanzania pia kuwaongezea fursa za kupata fedha na masoko,”
anasema Gutierrez
tangu
uzinduzi mpaka sasa Tigo imekuwa ikiwapa wajasiriamali hawa mafunzo
kuhusu mbinu za kupata mikopo na usimamizi wa biashara ili kuwajengea
uwezo wa kusimamia miradi yao kwa maslahi ya kwao na taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wakinamama wajasirimali, Happy Mabeba, anasema mpango mkakati wa
Tigo Tanzania ni faraja kubwa kwa wanawake nchini kwa sababu imemuondoa
katika dimbwi la umasikini na utegemezi kwenye familia yake.
Mabeba
anasisitiza kwamba kampuni ya Tigo Tanzania na mpango wao wa Wezesha
Wanawake kwa Maendeleo ni fursa pekee kwa wanawake nchini ambao tatizo
lao kubwa ni mitaji ya kuanzisha biashara mbalimbali.
“Kila
mwanamke angependa kuwa na maisha ya kumfanya kuishi bila kutegemea
zaidi kwa mwanaume, tumepokea vizuri mpango ule wa Tigo na
tunatunaendelea kusogea kutoka tuipokuwa hadi sehemu nyingine nzuri
zaidi,”
Na
Rose Rwejuna (33) anasema kwamba baada ya Tigo kuanzisha mpango mkakati
wa kusaidia wakinamama kupitia bidhaa yake ya Tigopesa maisha ya
wakinamama na wasichana wengi yamebadilika kwa kiasi kikubwa.
“baada
ya kufungua kibanda changu cha Tigopesa sasa ninaweza kusomesha watoto
wangu na kutunza familia bila matatizo yoyote , natoa shukurani za
kipekee kwa Tigo,” anasema
Anasema
kwamba kwa muda mrefu alikuwa hana kazi ya kufanya wala kipato cha
kuweza kujitunza na kutunza familia yake lakini baada ya kampuni ya simu
ya Tigo kuanza kusaidia wakinamama amepiga hatua kubwa sana kimaisha.
Zulfa
Omari ambaye anamiliki kibanda cha Tigo pesa maeneo ya manzese tip
top, anasema kwamba alipata mkopo kutoka Tigo Tanzania wa fedha taslimu
shilingi 300,000 na kuanza rasmi kazi yake ya uwakala mwaka jana mwezi
wa Oktoba na inakwenda vizuri.
“kwa
kweli napenda nachukua fursa hii adhimu kuwashukuru viongozi wote wa
kampuni ya simu ya Tigo kwa msaada wao kwa sababu kwa sasa naweza hata
kusomesha watoto wangu wawili mmoja sekondari na mwingine shule ya
msingi,” alisema.
Kwa
upande wake Dannis Minga yeye ni wakala wa Tigo pesa maeneo ya Ubungo
maziwa anasema kwamba alipata mkopo kupitia Tigo wa shilingi 300,000 na
kwa sasa ana mtaji wa shilingi milioni moja na lakin tano (1.5m) na
ameweza kufungua biashara nyingine ya vipodozi ambayo inamwingizia
kipato kwa ajili ya familia.
“yaani
sijui nisemeje! Tigo wamekuwa msaada mkubwa sana katika maisha yangu
binafsi kwa kunitoa kutoa sehemu moja kwenda nyingine na mshukuru Mungu
mwanangu anasoma bila matatizo shule ya msingi sasa,” aliongeza
Katika
kuadhimisha siku ya wanawake Jumamosi ya kesho kampuni hiyo ya Tigo
Tanzania watagawa zawadi mbalimbali kama mabegi, vocha za bure, T-shirts
na peni katika baadhi ya maduka yake kama vile Mlimani city, Tegeta
(Kibo Complex), Quality Mbagala shop, Kigamboni, Mbeya, Tanga na duka
jipya Mtwara.
0 comments:
Post a Comment