Harnaam
Harnaam Kaur, mwanamke mwenye umri wa miaka 23 anayeishi katika mji wa Slough, Kusini Mashariki mwa Uingereza amepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu asiowafahamu kwenye mitandao kwa sababu ya ndevu zake nyingi zinazomfanya asitofautishwe kirahisi na mwanaume.
Harnaam Kaur, mwanamke mwenye umri wa miaka 23 anayeishi katika mji wa Slough, Kusini Mashariki mwa Uingereza amepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu asiowafahamu kwenye mitandao kwa sababu ya ndevu zake nyingi zinazomfanya asitofautishwe kirahisi na mwanaume.
Mwanamke huyo ambaye anakabiriwa na tatizo la kuwa na vinyweleo vingi kupita
kiasi, tatizo linalojulikana kitaalamu kama ‘polycystic ovary
syndrome’, ameeleza kuwa alianza kupata tatizo hilo akiwa na umri wa
miaka 11 na kwamba alikuwa akizinyoa mara mbili kwa wiki.
Ameeleza
kuwa alipokuwa shuleni alikuwa akionewa sana kwa kuitwa majina mengi ya
kejeli kama ‘jike dume’, na kwamba alikuwa anashindwa hata kuwaangalia
watu usoni na alipotoka shule alijifungia ndani siku zote asionekane
mara kwa mara.
Ameongeza kuwa kutokana na kuishi katika hali hiyo alifikia hatua akafikiria kujiua.
Hata
hivyo, Harnaam amesema kuwa amejiunga na dini ya Sikh na kubatizwa, na
kwamba imani ya dini hiyo hairuhusu watu kunyoa vinyweleo vyao kwa kuwa
Mungu ndiye aliyewaumba hivyo. Kwa hiyo ameziachia nywele zake na sasa
anaonekana kama mwanaume akiwa na nywele nyingi kidevuni, mikononi na
kifuani.
Imani hiyo imempa ujasiri zaidi juu ya muonekano wake, na anajiona mwanamke mwenye mvuto zaidi.
“Nahisi
nimekuwa mwanamke zaidi, nina mvuto zaidi na nadhani naonekana hivyo
pia. Nimejifunza kupenda jinsi nilivyo na hakuna kitakachonitikisa sasa
hivi.” Amesema Harnaam.
“nawezza
kwenda kwenye maduka ya wanawake bila kuhisi kuwa sitakiwi kuwa kule.
Navaa skirts, gauni na vidani na napenda kutengeneza kucha zangu kama
msichana mwingine yeyote.
CHANZO: SOPHIE MBEYU BLOG
CHANZO: SOPHIE MBEYU BLOG
0 comments:
Post a Comment