SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, March 12, 2014

HUYU JAMAA NDIO MREFU KUSHINDA WOTE BONGO, HASHIM THABEET HAINGII..TAZAMA PICHA ZAKE


Huyu ni Baraka kijana mrefu kitanzania

Inasemekana ni kijana mrefu kuliko wote Tanzania. Kijana huyu (katikati pichani) ambaye anadhaniwa ni mrefu kuliko vijana wote Tanzania anaishi maeneo ya Gongolamboto, Banana jijini Dar es salaam. Kijana huyu huwa haonekani sana mitaani, lakini aliingia mjini siku hiyo na kuleta kizaa zaa kikubwa pale alipoibuka mitaa ya Aggrey, Kariakoo. Alikuwa kivutio kwa kila aliyemuona, alifunga mtaa watu wakimshangaa na kumgombania kupiga nae picha. Kila aliyetaka kupiga nae picha alitoa Shilingi elfu moja Tsh. 1000.
Picha hiyo amepigwa ndani ya Kinyozi (Salon) aliyoingia kupunguza nywele zake na umati wa watu walikuwa nje ya kinyozi huyo kumsubiri atoke. Mpaka sasa hajajulikana jina lake kamili na anafanya nini. Inasemekana kuna watu wanamfuatilia kumsaidia umaarufu.



Hapa Hasheem Thabit alipokutana na Baraka

JULIUS CHARLES

UKIMUANGALIA kwa mara ya kwanza mchezaji wa Tanzania anayecheza timu ya kikapu ya Oklahoma City Sounders inayoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), Hasheem Thabit unaweza kujiridhisha kwamba ni mrefu kuliko Watanzania wote uliowahi kuwaona. Ana futi 7.3.

Lakini mjini Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani kwenye shule ya Lord Barden yupo mchezaji anayemzidi Hasheem kwa urefu akiwa na futi 7.5. Si mwingine namzungumzia Julius Charles (18) ni maarufu zaidi maeneo ya Bagamoyo, na umaarufu huo umetokana na kimo chake huku wengi wakimuita mpinzani wa Hasheem Thabit kutokana na urefu alionao ambao umepitiliza na ukikutana naye lazima utishike au.......

CHANZO HIKI HAPA