SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, March 3, 2014

Lupita Nyong'o anyakua tuzo ya Oscar.

Muigizaji msaidizi katika Filamu ya 12 Years, Lupita Nyong'o akionyesha wazi hisia zake baada ya kushinda tuzo hiyo kwa muigizaji msaidizi bora zaidi. Alicheza kama msichana mtumwa ambaye alipendwa na bwenyenye wake.
Lupita Nyong'o:Nyota wa filamu '12 Years a Slave' alikuwa muigizaji msaidizi na baada ya kuteuliwa kwa tuzo hiyo, alifanikiwa kuinyakua katika hafla ya tuzo za Oscars
Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo la Oscar la mwigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masaibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''Baada ya kupokea tuzo hilo Lupita amesema " Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukran na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo la mwigizaji bora msaidizi wa kiume kwa jukumu lake la kuelezea maisha ya mwanamke aliye na jinsia mbili aliyekuwa na akiishi na virusi vya HIV katika filamu Dallas Buyers Club.Alilazimika kupunguza uzani kwa kipindi kifupi ili kuigiza.Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.

0 comments:

Post a Comment