SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, March 3, 2014

" BABA ANATAKA NIOLEWE, APATE NGOMBE, MIMI BADO MDOGO NA TENA NI KILEMA"


Moshi Hussein ambaye ni mlemavu wa viungo anayeishi nyumbani kwa baba yake mzazi huko katika kijiji cha Magiri wilaya ya Uyui mkoani Tabora,binti huyu ana umri wa miaka 13 hajawahi kupelekwa Shule kwa maana ya kupata haki kama wapatavyo watoto wengine,Moshi amekuwa akililia hilo kwa baba yake mzazi bila mafanikio.Jambo baya zaidi kwa mujibu wa maelezo ya Moshi baba yake anahitaji aolewe ili aweze kupata Ng'ombe licha ya kuwa ana umri mdogo na hawezi kukabiliana na Changamoto za ndoa kulingana na ulemavu alionao.
Moshi kwakuwa hana uwezo wa kutembea umbali hata wa hatua kumi anawaomba wasamalia wema kumsaidia mambo makubwa matatu,kwanza ikibidi kumuondoa nyumbani kwao ili aepukane na ndoa ya lazima,Pili apelekwe shuleni kwakuwa anaona kukaa kwa baba yake ni wazi kwamba atakuwa anatafuta umasikini mwingine wa ziada ukiachana huo wa ulemavu wa viungo ambao umekuwa kikwazo kikubwa hata cha kujihudumia masuala mengine ya kiutu wa mwanamke.Kwa mujibu wa maelezo yake Moshi ana mshangaa baba yake kwa uamuzi wa kutaka aolewe kwakuwa hata ndoa yenyewe haoni kama itakuwa na maana kutokana na ulemavu alionao na pia haoni sababu ya kuwa mzigo kwa mtu mwingine katika maisha yake.
Moshi amekuwa akijikatia tamaa kulingana na ulemavu alionao,"Kama ningekuwa na mama labda hata ningeweza kupelekwa shule na mimi ningekuwa msomi kama wengine,lakini kwa hali hii ni bora hata ningekufa nimfuate mama yangu huko aliko"

Via KapipiJHabari

0 comments:

Post a Comment