SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, February 5, 2014

TIGO YAZAWADIA MILIONI 830/- KWA WATEJA 2,335


Mshindi wa promosheni ya Tigo 'Shinda Kitita na Tigo Pesa' Bi. Germina Shayo (kushoto) akipokea mfano wa hundi wa shilingi milioni 10 kutoka kwa Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa Mary Rutta katika hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika mapema leo katika makao makuu ya Tigo, Makumbusho jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa Tigo ishazawadia fedha taslimu shilingi milioni 830 kwa wateja 2,335 nchi nzima.
Mshindi wa promosheni ya Tigo 'Shinda Kitita na Tigo Pesa' Bi. Germina Shayo akiwa ameshikilia mfano wa hundi wa shilingi milioni 10 kwa furaha baada ya kuibuka mmoja wa washindi 375 katika droo iliyofanyika wiki iliyopita. “Maisha na Tigo yamekuwa mazuri kupita maelezo!” alisema mfanyabiashara huyo wa nguo kutoka Moshi.
Tigo yazawadia milioni 830/- kwa wateja 2,335
Dar es Salaam, 5 Februari, 2014 – Ikiwa imebakia wiki moja kabla ya kumalizika kwa promosheni ya Cheza Kwa Furaha Unaposhinda Kitita na Tigo Pesa, kampuni ya Tigo imezawadia kiasi cha shilingi milioni 830/- wateja wapatao 2,335 kutoka sehemu mbali mbali nchini kwa kipindi cha miezi miwili.
Akitoa ufafanuzi kuhusu promosheni hiyo katika makao makuu ya Tigo leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa Mary Rutta, amesema aina ya zawadi zilizotolewa ni shilingi 200,000/- kwa wateja 50 kila siku, milioni mbili kwa wateja 20 kila wiki na zawadi ya juu kabisa ya shilingi milioni 10 wanayoshinda wateja watano kila baada ya wiki mbili.
“Tunazidi kushuhudia wateja wengi zaidi wakifurahia kushinda hizi zawadi za fedha taslimu kwa kufanya miamala kupitia akaunti zao za Tigo Pesa. Hii ni pamoja na kutuma fedha, kununua bidhaa, kuongeza salio au kulipia bili mbali mbali. Tunafuraha kwamba washindi wametoka mikoa yote nchini na kumekuwa na uwiano mzuri baina ya washindi kutoka mijini na vijijini,” alisema Rutta.
Mratibu huyo wa promosheni aliendelea kutoa wito kwa wateja wa Tigo kuendelea kufanya miamala ya Tigo Pesa akisisitiza kwamba imesalia wiki moja tu promosheni hii kuisha katikati ya mwezi Februari.
“Promosheni yetu inadhihirisha kwamba Tigo ni kampuni ambayo inaendelea kuweka jitihada ya kila siku katika kukidhi matarajio ya wateja wake. Tunaamini kuwa promosheni hii kwa namna moja au nyingine imeweza kubadilisha maisha ya washindi hawa 2,335 kama ambavyo wamekuwa wakishuhudia wenyewe,” alisema.
Rutta alitumia nafasi hiyo kuwakabidhi zawadi washindi wawili kati ya jumla ya washindi 375 waliopatikana katika droo ya promosheni hiyo iliyofanyika mwishoni wa wiki iliyopita. Waliokabidhiwa zawadi zao ni Bi. Germina Shayo aliyeshinda shilingi milioni 10 na Bi. Mariam Sawaya aliyejishindia shilingi milioni mbili.
“Maisha na Tigo yamekuwa mazuri kupita maelezo!” alisema Germina Shayo, mshindi wa zawadi ya juu kabisa.
Naye Sawaya aliwahimiza watanzania hasa wateja wa Tigo waendelee kutumia huduma ya Tigo Pesa ili kuweza kushinda. “Nilikuwa naomba kwamba siku moja niweze kushinda ha hakika na mimi leo nimebahatika. Yeyote anawaweza kushinda katika promosheni hii,” alisema.
Ili kupata nafasi ya kushinda katika muda uliobaki wa promosheni hii, Rutta aliwasihi wateja wa Tigo “kuendelea kutumia akaunti zao za Tigo Pesa kwa ajili ya kutuma fedha, kununua bidhaa, kuongeza salio au kulipia bili mbali mbali, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.”

0 comments:

Post a Comment