SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, February 6, 2014

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini-Chadema, Mchungaji Peter Msigwa amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Iringa

 MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (48) leo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Iringa akituhumiwa kwa kosa la kujeruhi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli.Kama anavyoonekana hapa kiwasalimu wafuasi wake mahakamani hapo 
MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (48)akiwa ndani ya mahakama
MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (48)akiteta na wakili wake Lwezaula Kaijage
 Chiku Abwao (MB) baada ya kumdhamini akitoka katika mahakama hiyo
Akisalimia wafuasi wake baada ya kutoka mahakamani kwa dhamana
---
 Na Francis Godwin Blog,Iringa
MBUNGE wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (48) leo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Iringa akituhumiwa kwa kosa la kujeruhi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli.
 
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elizabeth Swai alisema Mchungaji Msigwa alitenda kosa hilo Febrauri 5, 2014 katika kijiji cha Nduli, mjini Iringa.
 
Alisema Mchungaji Msigwa anashitakiwa kwa kumjeruhi Salum Kahita kinyume na kifungu kidogo namba 225 cha sheria ya kanuni za adhabu.
 
Akiwa amefunguliwa kesi ya jinai namba 28 ya mwaka 2014, Mchungaji Msigwa anayetetewa na wakili Lwezaula Kaijage alikana kosa hilo na hakimu aliahirisha kesi hiyo itakayotajwa tena Machi 10, mwaka huu kwa kile kilichoelezwa kwamba uchunguzi wake haujakamilika.
 
Pamoja na Mchungaji Msigwa, jeshi la Polisi limewapandisha kizimbani Meshack Chonanga (22) na Paulo Mapunda wote wakazi wa kijiji cha Nduli mjini Iringa  wakituhumiwa kumjeruhi Alex Mpiluka wakati wa kampeni hizo.
 
Watuhumiwa hao walirudisha mahabusu ya mahakama hiyo baada ya wadhamini wao kuchelewa kufika mahakamani hapo.
 
Kama ilivyokuwa kwa Mchungaji Msigwa, nao kila mmoja anatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaoweka dhamana ya ahadi ya Sh Milioni 2.

0 comments:

Post a Comment