SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Friday, February 14, 2014

Kwa Mnaofatilia Kandanda La Bongo, Hii Ndio Stori Mpya Inayomhusu Mchezaji Kabumbu Okwi Kwa Sasa.

Okwi 
Emmanuel Okwi ambae ni mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda aliyesajiliwa na klabu ya Yanga,  ameruhusiwa rasmi kikiwa ni kibali kutoka shirikisho la soka duniani (FIFA) kushiriki kuichezea timu yake ya sasa ambayo ni Yanga.
Okwi ambaye alikuwa amesimamishwa kutokana suala la mgogoro mauzo yake uliokuwa ukizihusisha timu zake za zamani Simba SC ya Tanzania na Etoile Du Sahel ya Tunisia, sasa ameruhusiwa kuitumikia Yanga huku FIFA ikiendelea kufuatilia kiundani kuhusu deni la Simba la dola 300,000 wanaloidai Etoile.
Fedha hiyo ilikuwa ya uhamisho wa mchezaji huyu kutoka Simba kwenda Tunisia takribani miaka miwili iliyopita ambapo baada ya kupata greenlight, Okwi sasa ataweza kuitumikia Yanga katika michuano ya ligi kuu na kombe la klabu bingwa ya Afrika.
NA MIRLADAYO.COM

0 comments:

Post a Comment