Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuzindua shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, wakati wa
hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar jana Jan 10, 2014.
Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamhuna. (Picha
na OMR).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la Msingi la shule ya Sekondari
ya Kiembe Samaki, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa shule hiyo
iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe
Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipokuwa akitembelea chumba cha
Maabara baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi
iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipotembelea katika chumba
cha Mawasiliano na mafunzo ya Kompyuta cha shule hiyo, baada ya uzinduzi
rasmi wa shule hiyo uliofanyika jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikagua moja ya vitabu vya kumbukumbu za Maktaba ya Shule mpya ya
Sekondari ya Kiembe Samaki wakati alipotembelea chumba hicho cha Maktaba
baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika
shuleni hapo mjini Zanzibar jana Jan 10, 2014. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa
shule hiyo, Amina Salum Khalfan.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitembelea chumba cha Maabala kati ya vyumba vinne vilivyopo shuleni
hapo.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Kiembe Samaki, wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kiembe
Samaki, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika jana Jan 10,
2014, mjini Zanzibar. (Picha na OMR).
0 comments:
Post a Comment