SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, December 25, 2013

Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania: Upepo mkali pamoja na mawimbi makubwa vinatarajiwa katika maeneo yote ya ukanda wa pwani.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

 Simu: 255 22 2460735/2460706
 FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
 Barua pepe:
met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
 Tovuti:
www.meteo.go.tz
 Unapojibu tafadhali nakili:
 Kumb. Na.: TMA/1622 24 Desemba, 2013 ---
 Taarifa Na.201312-05
 Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki Saa 3 Asubuhi
 Daraja la Taarifa: Angalizo
 Kuanzia:Tarehe 25 Desemba, 2013
 Mpaka: Tarehe 26 Desemba, 2013
 
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
 Upepo mkali kufikia kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa kuzidi mita 2.0 vinatarajiwa katika ukanda wote wa pwani.
 
 Kiwango cha uhakika:Wastani (60%)
 Maeneo yatakayoathirika Mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
 
 Maelezo:
 Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi, karibu na visiwa vya Comoro. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutokea pwani ya Somalia.
 
 Angalizo:
 Wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
 
 Maelezo ya Ziada
 Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo.
 
Imetolewa na
 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
.

0 comments:

Post a Comment