SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, December 18, 2013

Rais Jakaya Kikwete Atuma salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo kufuatia vifo vya watu wawili vilivyotokea tarehe 15 Desemba, 2013 katika Kitongoji cha Kanyama Kata ya Kisesa Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza.


Rais Jakaya Kikwete
---

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo kufuatia vifo vya watu wawili vilivyotokea tarehe 15 Desemba, 2013 katika Kitongoji cha Kanyama Kata ya Kisesa Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza.

Rais ametuma salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa kufuatia vifo vya BW. Clement Mabina na Tenery Malimi vilivyotokea baada 
vurugu zilizosababishwa na mabishano ya ardhi.

Rais amemuomba Mkuu wa Mkoa kuwatahadharisha wananchi kutokuchukua sheria mikononi mwao na pia kuwa waangalifu na matumizi ya silaha za moto.

“Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na taarifa za vifo vya wananchi hao wawili (2) vilivyosababishwa na mgogoro wa Ardhi ambao ungeweza kupata suluhu kwa njia za amani. Ni vema wananchi kuwa na subira na kuwa waangalifu katika kutatua migogoro yao”. Rais amesema na kuongeza kuwa “ ni vema subira na busara zikawa ndio muongozo wa kutatua migogoro yetu katika jamii badala ya hasira”.

Aidha, Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Mkoa amfikishie salamu zake za dhati kwa familia na ndugu wa Marehemu Mabina pamoja na Wazazi na ndugu wa Marehemu Tenery Malimi, ambao walifariki kutokana na vurugu hizo.

“Amewaomba familia zote mbili ziwe na subira wakati huu mgumu kwa kuondokewa na wapendwa wao na kuviacha vyombo vya dola kuchukua hatua kwa kufuata taratibu zilizopo”. Kwa ndugu Mabina, Chama cha Mapinduzi kimepoteza mmoja wa viongozi wake mahiri na wa kutumainiwa. Aidha, kwa marehemu Tenery taifa limepoteza mmoja wa vijana wake wanaochipukia ambae angejaaliwa kuishi angeweza kutoa mchango muhimu kwa maendeleo ya jamii na nchi yetu.

Mabina amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Diwani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Magu mwaka 2000 – 2005, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, mwaka 2007 – 2012.

Rais ameziombea nyoyo za marehemu wote Mungu azilaze mahali pema peponi Amen.
Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

0 comments:

Post a Comment