Mratibu
wa Promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akichezesha
droo ya wiki ya tano ya Pambika na Samsung kutafuta washindi 15, kulia
ni msimamizi toka bodi ya kusimamia michezo ya bahati nasibu Tanzania
Bw. Bakari Maggid kifuatilia kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na
washindi wanapatikana kwa njia sahihi. Kushoto ni Meneja Mauzo na
Usambazaji wa Samsung Tanzania.
Mratibu
wa Promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew na mmoja ya
washindi wa droo ya tano ya Pambika na Samsung wakati wa kuchezesha droo
ya tano. Jumla ya washindi 75 wameshapatikana toka kuanza kwa
promosheni ya Pambika na Samsung katika kipindi cha wiki tano tangu
kuanza kwa promosheni Septemba 7, 2013, promosheni hiyo inatarajiwa
kuisha tarehe Desemba 23, 2013 ambapo mteja mmoja ataondoka na gari
jipya aina ya Mitsubishi Double Cabin.
Akizungumza
na wanahabari Meneja wa Samsung Tanzania kitengo cha mauzo na
Usambazaji Bw Sylvester Manyara aliwahimiza watanzania kuzidi kununua
bidhaa halisi na kuzisajili katika mfumo wa dhamana ya ziada na kuingia
kwenye droo ambapo bado nafasi ya kushinda zawadi kubwa ya Mitsubishi
Double Cabin ipo wazi katika droo itakayofanyika Jumatatu ya wiki ijayo
katika maegesho ya magari ya Mlimani City, Dar es salaam.
Promosheni
ya wiki sita ya pambika na Samsung inayoendelea imetangaza majina ya
washindi wa droo ya tano katika droo ya wiki hii iliyofanyika makao
makuu ya Samsung na kushuhudia wateja 15 wakijishindia zawadi mbalimbali
na kufanya jumla ya wateja 75 kuzawadiwa ndani ya wiki tano tangu
kuanza rasmi kwa promosheni hii Septemba 7, 2013.
Samsung
itafunga pazia la mwisho la promosheni ya Pambika na Samsung wiki ijayo
Jumatatu ya Desemba 23, 2013 ambapo mteja mmoja mwenye bahati ataweza
kujiondokea nyumbani na zawadi kubwa ya gari aina ya Mitsubishi Double
Cabin itakayosheheni bidhaa zote zilizokuwa zikitoka kila wiki toka
Samsung.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa droo ya tano ya kila wiki ya Pambika
na Samsung, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania Bw Sylvester
Manyara aliwahimiza watanzania kuwa makini na bidhaa feki kwani
zinaharibu thamani ya maisha yao na badala yake waendelee na utamaduni
wa kununua bidhaa halisi na kuzisajili hata mara baada ya kumalizika kwa
promosheni ya Pambika na Samsung
Manyara
alisema kuwa “Sisi Samsung tumefurahishwa na mwenendo mzima wa droo za
kila wiki zinazofanyika chini ya uangalizi na sheria za Bodi ya michezo
ya kubahatisha, tukiwa tunaelekea katika droo yetu ya mwisho ya kutoa
zawadi kubwa kabisa ya gari ambayo ni Mitsubishi Double cabin
iliyoseheni bidhaa za Samsung, naomba nimuhamasishe kila mtu kuendelea
kununua na kusajili bidhaa halisi za Samsung kutoka kwenye maduka yetu
au mawakala waliothibitishwa na Samsung wanaopatikana nchi nzima”.
“Lengo
letu kuu si kuongeza mauzo ya bidhaa zetu ila ni kutengeneza jukwaa
litakalohamasisha watanzania wote kufahamu tatizo la bidhaa feki zilizo
sokoni, Samsung ina jukumu hili la kijamii la kuwalinda wateja wake
kutokana na bidhaa feki, tumeleta Pambika na Samsung ili kubadili maisha
ya wateja na kuwafanya wawe na furaha pamoja na familia zao pale
wanaponunu bidhaa halisi na kuzisajili katika mifumo yetu ya dhamana
ambao haipatikani kwenye bidhaa feki” alielezea Bw Manyara.
Baadhi
ya washindi wa wiki hii waliojishindia zawadi mbalimbali ni Adam
Kennedy Manene (17) Mwanza ambae ni Mwanafunzi wa Shule ya sekondari
aliyejishindia deki ya DVD, Kija Shija (22) kutoka Dodoma aliyejishindia
Muziki wa nyumbani, mwengine ni kutoka Mbeya aliyejishindia deki ya DVD
Docus Moses (22) mfanyabiashara wa jijini Mbeya na Shamasa Said Hamis
toka Arusha aliyejishindia zawadi Muziki wa Nyumbani.
“Bidhaa
za Samsung zina ubora wa kimataifa na zinahakikisha ubora huo kwa
kudumu muda mrefu lakini kuna bidhaa feki sokoni ambapo changamoto yake
ni ugumu wa kutofautisha na bidhaa halisi, mamlaka husika pamoja na
wadau wakubwa tunatakiwa kufanya kazi ya ziada katika kumkomboa mtumiaji
wa mwisho aweze kufurahia thamani ya bidhaa anayonunua” alimalizia Bw
Manyara
Toka
kuanza kwa Pambika na Samsung tayari imeshazawadia wateja mbalimbali 75
ambapo zawadi zilizotoka ni Kompyuta mpakato 5, Majiko ya kupashia
chakula 15, Luninga za LED 32’, muziki wa nyumbani 16, Samsung Galaxy
Tab 3, mashine za kufulia nguo 2, jokofu 3, na deki za DVD 27 ndani ya
wiki tano kwa washindi toka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dar es
salaam, Dodoma, Tabora, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro na Kilimanjaro.
Kuingia
kwenye droo na kujihakikishia nafasi ya kushinda, mteja atatakiwa
kununua simu yoyote halisi ya Samsung na kuisajiili katika mfumo wa
dhamana ya ziada kwa kutuma nambari za utambulisho wa simu hiyo yaani
namba za “IMEI” kwenda 15685, na kwa wale watakaonunua bidhaa nyengine
watatakiwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika maduka yote ya
Samsung ambapo wataingia kwenye droo na kuwa na nafasi ya kushinda
zawadi kubwa ya Mitsubishi Double Cabin katika droo ya mwisho
itakayofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu ya
Desemba 23, 2013.
0 comments:
Post a Comment