Meneja
Mkazi wa Uchumi Supermarket Chriss Lenana (kushoto) na Ofisa Mkuu wa
Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh wakikata utepe
kuzindua rasmi duka la Vodacom ndani ya Uchumi Supermarket ikiwa ni
huduma ya kwanza na ya kipekee nchini. Duka hilo linawawezesha wateja wa
Vodacom kupata huduma za kampuni ikiwemo moderm, vocha, usajili wa
nambari zao, M-pesa n.k wanapofika kwenye Supermarket hiyo kwa ajili ya
kupata kufanya manunuzi ya mahitaji mengine
.
.
Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh akiongea
na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa duka la Vodacom ndani
ya Supermarket ya Uchumi. Vodacom imezindua pia huduma za malipo kwa
M-pesa kwa wateja wanaofanya manunuzi ndani ya Supermarket hiyo. Kushoto
ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh akitumia
huduma ya M-pesa kulipia bidhaa alizonunua ndani ya Supermarket ya
Uchumi ya jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa
huduma hiyo. Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum
Mwalim, Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Chriss Linana. Wa kwanza
kulia ni Mkuu wa Huduma za Maduka ya Vodacom Upendo Richard.
.Vodacom yazindua pia duka ndani ya duka la Supermarket
.Kupunguza usumbufu kwa wateja
Katika
muendelezo wa mapinduzi ya kuyaleta maisha kiganjani, sasa wateja
wanaofika kupata huduma kwenye SuperMarkert ya Uchumi lililopo katika
jengo la Quality Center jijini Dar es salaama wanauwezo wa kulipia
huduma zao kwa njia ya M-pesa.
Aidha,
Vodacom pia imefungua duka la huduma kwa wateja wake ndani ya
Supermarket hiyo ikiwa ni ubunifu wa aina yake hapa nchini na hivyo
kuwapa nafasi ya kipekee wateja wa Vodacom kumaliza mahitaji yao yote
kwa nwakati mmoja.
“Tunazidi
kuongoza katika ubunifu hili ni jambo tunalolipa kipaumbele kw alengo
la kuhakikisha tunatoa nafasi kwa wateja wetu kufaidi matumizi ya
teknolojia na kubadili maisha yao, hakuna shaka kila tunachokifanya
kinawatimiza matarijio yao kwetu.”Alisema Ofisa Mkuu wa Mauzo na
Mahusiano wa Vodacom
Kila
mmoja Wakati huu w amsimu wa siku kuu angependa kuona anatumia muda
mfupi na kwa urahisi zaidi kupata huduma, hatua moja muhimu ni
kuwawezesha kuwa na njia rahisi na nyepesi zaidi ya kukamilisha mahitaji
yao na hivyo ndivyo tunavyofanya leo kwa kuwatanagzi wateja wetu
kutumia M-pesa wanapofika Uchumi SuperMarket.”Aliongeza
Kwa
sasa M-pesa inawaunganisha wateja wetu na biashara zaidi ya 300 katika
Nyanja mbalimbali ikiwemo kulipia tiketi za ndege ving’amuzi,LUKU, maji,
kutoa na kuweka fedha katika akaunti za benki zaidi ya 20 na hivyo
kuongoza soko miongoni mwa huduma za fedha kwa njia ya simu.. Kwa upande
wake Meneja Mkazi wa Uchumi Supermarket Tanzania, Chriss Lenana
amebainisha kuwa ni jambo la furaha na kujivunia kuzinduliwa kwa ubia
huo kati ya kampuni yake na Vodaco na hivyo kuwawezesha wateja wake
kutumia simu zao kwa ajili ya malipo ya manunuzi.
“Kufunguliwa
kwa duka la Vodacom hapa kwetu kutasaidia sana wateja wetu si tu kuweza
kupata huduma za M – PESA bali pia huduma nyingine za kimawasiliano na
hatimaye kuepukana na matatizo ya kimawasiliano yanayowakabili.
Tunapokea idadi kubwa ya wateja kila kukicha na kwa kufunguliwa kwa duka
hili Vodacom wamefanya suala la msingi ambapo awali iliwalazimu wateja
kusafiri mpaka makao makuu kufuata huduma hizo kitu ambacho ni usumbufu
na kiusalama ni changamoto.” Alisema Lenana
“Huduma
hii ya malipo kwa njia ya M-pesa tutaisamabza kwenye maduka yetu yote
ambayoyapo kwenye mipango yetu ya mwaka 2014/2015, ni wazi tumewaptia
wateja wetu kitu kizuri na tunawaomba watumie njia hii ya malipo kwa
kujiamini kwani mteja hupatiwa pia stakabadhi ya mununizi”Aliongeza.
Duka
hilo ni moja kati ya maduka 200 ya Vodacom ambayo yapo mbioni
kufunguliwa nchi nzima na pia ni muendelezo wa uboreshwaji wa huduma ya M
– PESA na huduma nyinginezo za kampuni hiyo nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment