Rais Jakaya Kikwete akimfaliji Mke wa marehemu Dk
Sengondo Mvungi, Anna Shayo, nyumbani kwa marehemu, eneo la Kibamba jijini Dar
es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph
Warioba akitia saini kitabu cha maombelezo ya kifo cha Mjumbe wa Tume hiyo Dkt.
Sengondo Mvungi nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akibadilishana mawazo na
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto)
nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi walipokwenda kuipa pole familia.
Kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph
Warioba wakifurahia jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe
(kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na
Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) walipokutana
nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi Kibamba jijini Dar es
Salaam.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Richard Lyimo
akimpa pole mke wa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi wakati Wajumbe
wa Tume walipokwenda kumpa pole.Picha na Tume ya Katiba
-----
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi
kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi
aliyefariki nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili
nchini siku ya Ijumaa, Novemba 15, 2013.
Baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika
Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Aidha, siku ya Jumamosi, Novemba 16, 2013 kutafanyika
Ibada ya mazishi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam
kuanzia saa 4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya
Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16,
2013.
Aidha, Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa
siku ya Jumapili, Novemba 17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani
Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu,
Novemba 18, 2013.
Dkt. Mvungi alifariki juzi (Jumanne, Novemba 12, 2013)
katika Hospitali ya Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini
alikopelekwa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha
Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake
Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya
kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3,
2013.
Wakati huohuo, Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba leo (Jumatano, Novemba 13,
2013) wameungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kufika nyumbani kwa marehemu Dkt. Mvungi eneo la Kibamba
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa
marehemu Dkt. Mvungi.
RATIBA YA SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA DKT. SENGONDO MVUNGI KESHO
MUDA
|
TUKIO
|
LEO, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK
NYERERE
| |
Saa 12:50 jioni
|
Kuwasili kwa
mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN
|
KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE
| |
Saa 2:00 – 3:30
asubuhi
|
Kuwasili kwa
Wageni, Wananchi na Waombolezaji
|
Saa 3:30 asubuhi
|
Kuwasili Mwili
wa Marehemu
|
Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
|
Ibada ya Misa
Takatifu, Viwanja vya Karimjee
|
Saa 5:45 – 6:55
mchana
|
Salaam za
Rambirambi na Neno la Shukurani
|
Saa 6:55 – 8:40
Mchana
|
Kuaga Mwili wa
Marehemu
|
Saa 9:00 Alasiri
|
Msafara kupeleka
mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi
|
KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU
- KIBAMBA, MSAKUZI
| |
Saa 2:30 – 4:30
asubuhi
|
Ibada ya Misa
nyumbani kwa marehemu
|
Saa 5:00 asubuhi
|
Kuanza safari ya
kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro
|
0 comments:
Post a Comment